WANYAMA 380 wamekufa kwa kugongwa na magari
ndani ya mwaka mmoja 2019 katika eneo la mapito ya wanyama kuanzia
Magugu wilayani Babati hadi Makuyuni
wilayani Monduli ambayo husaidia wanyama kwenda hifadhi ya tarangire na hifadhi
ya Manyara.
Mtafiti
wa wanyamapori katika mradi wa Simba Tarangire, Dk Bernard Kissui alitoa
taarifa hizo juz katika kikao cha kujadili kuokoa eneo la mapito ya wanyama kwa
kuchinja hadi Mdori ambalo linaendelea kuvamiwa .
Dk
Kissui alisema kati ya januari hadi Desemba 2019, wamebaini wanyama 380
kugongwa katika barabara hiyo hali ambayo inatishia uhai wa hifadhi za taifa za
Tarangire na Manyara.
Alisema
katika eneo hilo ,licha ya wanyama kugongwa pia kuna uvamizi mkubwa wa
wananchi, kulima na kuweka makazi ndani ya eneo hilo.
“Kama
serikali isipochukuwa hatua sasa, wanyama wengi watapotea lakini pia tutaathiri
ikolojia ya Tarangire na Manyara”alisema
Alisema
wanyama hao, wanagongwa wengi nyakati za
usiku hasa kutokana na mwendokasi ya magari.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantite Kanyasu, aliagiza Shirika la hifadhi
za Taifa(TANAPA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Wanyamapori(TAWA) na Taasisi
ya Utafiti wanyamapori(TAWIRI), kuandaa mabango na kuweka katika eneo la
barabara hiyo kutoka Arusha hadi Babati.
“naagiza
kuwekwa mabango ya kuonesha faini ukigonga mnyama mfano simba dola 4000,pia
yawekwe mabango ya kupunguza mwendo kwa kuonesha wanyama wanaovuka maeneo hayo”alisema
Alisema
pia atazungumza na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,ili kuhakikisha zinawekwa alama
za kupunguza mwendo za kisasa ambazo haziwezi kuisha kwa muda mfupi.
Mkurugenzi
wa utafiti wa TAWIRI, Dk Julius Keyyu alisema ili kuokoa wanyama na mapito yao
ni muhimu kuwepo ushirikiano baina ya wananchi, viongozi wa vijiji na wadau wa
utalii.
Dk
Keyyu alisema tayari taasisi kadhaa zimekuwa zikifadhili mradi wa kufatilia
wanyama, ikiwepo taasisi ya Chemchem Foundation ambayo imegharamia mradi wa
Tembo katika eneo hilo kufungwa vifaa vya mawasiliano kufatilia mapito yao.
Akizungumzia taaarifa hiyo,Mkurugenzi wa Wanyamapori
nchini, Dr Maurus Msuha alisema ni lazima sasa serikali kwa kushirikiana na
wadau kuchukuwa hatua za kulinda eneo hilo la mapito ya wanyama.
alisema
Katika kulinda eneo hili ni lazima barabara kuwekwa alama na kutolewa adhabu
kwa wanaogonga wanyama lakini pia katika kulinda mapito ya wanyama wananchi
wanapaswa kushirikishwa ili kupisha maeneo ya mapito ya wanyama.
Post A Comment: