Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha NCCR – Mageuzi taifa Edward Simbeye akizungumza wakati wa kupokea wanachama wapya katika Jimbo la Shinyanga leo Jumatano Mei 20,2020 katika ofisi ya NCCR - Mageuzi Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde
Kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Shinyanga Mjini, Charles Shigino akitangaza kuhamia Chama Cha NCCR – Mageuzi. Kulia ni aliyekuwa Katibu wa Chadema ni msingi Kanda ya Serengeti na Operation Kamanda Chadema ni Msingi katika Majimbo ya Solwa,Kongwa na Temeke Bi. Eunice Kanumba ambaye naye amejiunga NCCR - Mageuzi leo.
Aliyekuwa Katibu wa Chadema ni msingi Kanda ya Serengeti na Operation Kamanda Chadema ni Msingi katika Majimbo ya Solwa,Kongwa na Temeke Bi. Eunice Kanumbaakitangaza kuhamia Chama Cha NCCR - Mageuzi.
Aliyekuwa Katibu wa Chadema ni msingi Kanda ya Serengeti na Operation Kamanda Chadema ni Msingi katika Majimbo ya Solwa,Kongwa na Temeke Bi. Eunice Kanumba akionesha Katiba ya chama Cha NCCR - Mageuzi aliyodai inazingatia utu.
Aliyekuwa Katibu wa Chadema ni msingi Kanda ya Serengeti na Operation Kamanda Chadema ni Msingi katika Majimbo ya Solwa,Kongwa na Temeke Bi. Eunice Kanumba akikabidhi kadi za Chadema kwaMkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha NCCR – Mageuzi taifa Edward Simbeye (kulia).
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha NCCR – Mageuzi taifa Edward Simbeye (kulia) akimkabidhi Katiba na Kadi ya NCCR - Mageuzi aliyekuwa Katibu wa Chadema ni msingi Kanda ya Serengeti na Operation Kamanda Chadema ni Msingi katika Majimbo ya Solwa,Kongwa na Temeke Bi. Eunice Kanumba.
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha NCCR – Mageuzi taifa Edward Simbeye (kulia) akimkabidhi Charles Shigino Kadi ya NCCR - Mageuzi.
Wanachama wapya wa NCCR - Mageuzi wakila kiapo.
Wanachama wapya wa NCCR - Mageuzi wakila kiapo.
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha NCCR – Mageuzi taifa Edward Simbeye akielezea kuhusu mikakati mbalimbali inayofanywa na NCCR - Mageuzi katika kuifanya Kanda ya Ziwa ya Bluu 'Kuimarisha Ngome ya NCCR - Mageuzi'.
Na Kadama Malunde
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Shinyanga Mjini, Charles Shigino na aliyekuwa Katibu wa chadema ni msingi Kanda ya Serengeti na Operation Kamanda Chadema ni Msingi katika Majimbo ya Solwa,Kongwa na Temeke Bi. Eunice Kanumba wametangaza kuhamia Chama Cha NCCR – Mageuzi na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha NCCR – Mageuzi taifa Edward Simbeye.
Charles Shigino na Eunice Kanumba ni miongoni wa wanachama wapya zaidi ya 90,000 kutoka Mikoa ya Mara na Shinyanga ambao wamejiunga na Chama cha NCCR – Mageuzi katika Mkakati wa Kuifanya Kanda ya Ziwa kuwa ya Bluu ‘Ngome ya NCCR – Mageuzi’.
Wakitangaza kujiunga na Chama cha NCCR – Mageuzi, Eunice Kanumba na Shigino wamesema CHADEMA imepoteza mwelekeo hivyo wameona ni vyema kujiunga na NCCR – Mageuzi kwamba ina demokrasia ya kweli.
“Nimetafakari sana na kuamua kujiunga NCCR – Mageuzi kwani ndiyo chama ambacho naona sasa kina Demokrasia ya kweli na viongozi wake wanafuata katiba ya Chama tofauti na CHADEMA ambayo viongozi wake hawafuati katiba ya Chama. Dira ya Chama cha Siasa ni Katiba kama katiba haifuatwi basi hicho siyo Chama tena”,alisema Shigino.
Shigino alisema sasa anaelekeza nguvu zote NCCR – Mageuzi ili kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kisiasa ikiwemo kutia nia ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini.
“Nimeipigania sana CHADEMA, hata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nilikuwa mstari wa mbele kama katibu Mwenezi jimbo la Shinyanga Mjini,haiwezekani nipiganie chama halafu nizarauliwe kirahisi tu. Nimekuja NCCR – Mageuzi na wapo wengi wananifuata,nitaitumikia NCCR –Mageuzi kwa moyo wangu wote”,aliongeza Shigino.
Naye Eunice Kanumba ambaye alikuwa Katibu wa kamati ya CHADEMA ni Msingi Kanda ya Serengeti alisema amejiunga na NCCR- Mageuzi kutokana na CHADEMA kutawaliwa na makundi mbalimbali yanayokigawa chama hicho.
“Najiunga na NCCR – Mageuzi ili niendelee na siasa za utu. Chadema haijali utu hata katika hili Janga la Ugonjwa Corona, Chadema haipo pamoja na serikali,wao kazi ya ni kutafuta idadi ya vifo vinavyotokana na Corona na kutoa taarifa kwa nia ovu,sijaona Chadema wakitoa hata Barakoa”,alisema Kanumba.
“Demokrasia ndani ya Chadema imepotea,Mwenyekiti wa Chadema Taifa anaendesha chama vile anavyotaka yeye. Ni ubabe tu na sijapenda vile wabunge wa CHADEMA wanavyofanyiwa,mfano hivi karibuni wakati Bunge la Bajeti likiendelea Mbowe aliwakataza wabunge kuingia Bungeni kwa hofu ya Corona na wale walioingia wakafukuzwa uanachama”,aliongeza Kanumba.
Akiwapokea wanachama hao wapya Mratibu Uenezi na Mahusiano ya Umma wa Chama cha NCCR – Mageuzi taifa Edward Simbeye aliwakaribisha wanachama hao na kuelekeza kuwa NCCR – Mageuzi ipo katika mkakati wa kuifanya Kanda ya Ziwa kuwa ya Ngome ya NCCR – Mageuzi.
“Leo tumepokea wanachama wapya 9 na kuwakabidhi kadi katika Mkutano na waandishi wa Habari ikiwa ni sehemu ya zoezi la kuimarisha chama. Tayari tumepokea wanachama zaidi ya 90,000 katika mkoa wa Mara na Shinyanga kutoka vyama mbalimbali vya siasa ndani ya miezi mitatu kupitia zoezi la kupata wanachama tunalolifanya kimya kimya. Shinyanga tumepata wanachama zaidi ya 42,000 na Mara zaidi ya 48,000 ambao tuna orodha ya majina yao na namba zao za simu”,alisema Simbeye.
Kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, Simbeye alisema NCCR – Mageuzi itasimamisha mgombea Urais na Ubunge huku akisisitiza kuwa NCCR- Mageuzi itaendelea kuikosoa serikali kwa staha kwani kukosoa na kukosolewa ni sehemu ya uongozi.
Post A Comment: