Hospitali na vituo vya afya vinapambana kuongeza nguvu kazi katika sekta ya afya katika kukabiliana na janga la corona.
Hitaji la watoa huduma za afya limekuwa kubwa kufuatia idadi kubwa ya waathirika wa virusi vya corona kwenye hospitali na vituo vya afya.
Mchango wa kila mmoja katika sekta ya afya unahitajika katika kuhakikisha nchi inapita salama katika kipindi hiki kigumu.
Mchango wa kila mmoja katika sekta ya afya unahitajika katika kuhakikisha nchi inapita salama katika kipindi hiki kigumu.
Baadhi ya nchi zimekwenda mbali kwa kuwarudisha madaktari wastaafu na hata kuwatumia walikuwa katika mwaka wa mwisho wa kuhitimu ili kukabiliana na upungufu wa watoa huduma za afya.
Kwa upande wa Tanzania hivi karibuni ajira 6000 za madaktari zilitangazwa kwa lengo la kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya corona.
Kama moja ya jukwaa la huduma za rasilimali watu nchini Tanzania, BrighterMonday Tanzania imechukua hatua kadhaa kuhakikisha sekta ya afya inaendelea kuwa na wataalamu wa kutosha kusaidia mapambano dhidi ya janga la corona.
“Tunaelewa kwamba mamilioni ya wafanyakazi ulimwenguni kote wameathiriwa na mlipuko wa COVID-19. Sekta ya afya imeathiriwa zaidi na janga hili.
Hii ndiyo sababu BrighterMonday Tanzania tumeendelea kutoa mchango wetu wa hali na mali kwa sekta ya afya na sekta nyingine zote zilizopo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya coroa.
Moja ya hatua muhimu ni kuanzisha programu ya Umoja Wakati wa Shida ambayo inawapa waajiri nafasi ya kutumia jukwaa letu bure na kupata huduma muhimu za rasilimali watu kwa punguzo kubwa”, anasema Reshma Bharmal-Shariff, Mkurugenzi Mkuu wa BrighterMonday Tanzania.
“Huu sio wakati ambao sekta ya afya inapaswa kuhofia suala la kupata nguvu kazi. Nguvu na akili zao zinapaswa kuelekezwa katika kupambana na janga la corona wakati tukiwasaidia kupata ‘askari’ sahihi watakaoongeza nguvu katika mapambano. Kwa kutumia teknolojia ya Best Match waajiri wanaweza kuajiri kwa ufasaha na kwa muda sahihi”, ameongeza Reshma.
Kwa kutumia teknolojia ya Best Match, wataalamu wa afya wenye uwezo na wanaoendana na mahitaji watachanguliwa kulingana na nafasi husika na watapewa kipaumbele katika mfumo ili kupunguza usumbufu kwa waajiri.
“Matumizi ya teknolojia ya Best Match yatapunguza usumbufu kwa waajiri ambao walipaswa kutumia muda mwingi kuchagua wataalamu ambao wanafaa kutokana na nafasi husika.
Waajiri wanaweza kutumia muda huo kufanya majukumu muhimu ya kupambana na janga la corona wakati BrighterMonday tukiwasaidia kupata wataalamu sahihi. BrighterMonday Tanzania itawasaidia waajiri kupata walau wataalamu 10 katika siku saba za kuweka tangazo la ajira”, amesema Reshma.
Post A Comment: