Waumini Marafiki wa Mtakatifu Rita wa Kashia, Kanisa Katoliki Jimbo la Singida wakiwa kwenye maombi ya Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwenye Kituo cha Hija kwa Bikira Maria kilichopo Kijiji cha Sukamahela WIlaya ya Manyoni mkoani hapa jana, kwa namna anavyoendelea kulilinda Taifa dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Kaimu Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani (mbele) Aliyemuakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Dkt.Rehema Nchimbi akiongoza Waumini kwenye maombi hayo.
Maombi yakifanyika mbele ya Sanamu ya Bikira Maria.
Waumini wakiandamana kuelekea kwenye maombi hayo.
Maombi yakiendelea.
Ndahani akiongoza tafakari wakati wa maombi hayo.
Mwenyekiti wa WAWATA Jimbo Katoliki la Singida, Veronica Mwambuta akiongoza sala maalumu ya shukurani.
Sister Maria Subi akizungumza wakati wa maombi hayo.
Maombi yakiendelea.
Mwakilishi wa Wanavyuo mbalimbali waliopo ndani ,ya Mkoa wa Singida kutoka Chuo cha St Joseph Dar es Salaam, Lucas Stephano akitoa ombi maalumu dhidi ya Corona.
Maombi yakiendelea.
Muonekano la eneo la Hija la Sukamahela.
Mandhari ya eneo hilo.
Ujenzi wa Kanisa lililopo katika kituo hicho cha Hija ukiendelea.
Na Godwin
Myovela, Singida
Na Godwin
Myovela, Singida
KAIMU Afisa
Vijana wa Mkoa wa Singida, Mwalimu Frederick Ndahani ameongoza waumini wa Kanisa
Katoliki ambao ni marafiki wakubwa wa Mtakatifu ‘Rita wa Kashia’ mkoani hapa
kwenye maombi maalumu ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea
kuwalinda na kuwaepusha watanzania dhidi ya madhara yatokanayo na janga la
Covid- 19
Ndahani,
ambaye alimwakilisha Mkuu wa , Dkt. Rehema Nchimbi kwenye kusanyiko la maombi hayo
yaliyofanyika jana eneo la Sukamahela, wilaya ya Manyoni mkoani hapa,
linalosadikiwa kuwa kati kati ya Tanzania, eneo ambalo Kanisa Katoliki limejenga
kituo cha hija kwa heshima ya Bikira Maria
“Tumekuja hapa
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea kulipigania taifa letu kupitia
maombezi ya Bikira Maria dhidi ya janga la corona. Na tumeamua kufanya maombi yetu
eneo hili kwa sababu lipo katikati ya nchi na ndio kitovu…lakini zaidi mama huyu
yupo hapa na kwa maombezi yake anaendelea kuimarisha ulinzi wa taifa letu,”
alisema Ndahani
Ndahani ambaye
ni miongoni mwa vijana walioshiriki kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2017, katika hotuba
yake amemfananisha Rais John Magufuli na Nabii Musa kwa namna anavyoongoza taifa
kwa unyenyekevu na maono ya kimungu huku nchi ikishuhudia miujiza mikubwa katika
kipindi hiki kigumu.
Kijana huyo
ambaye amekuwa na juhudi kubwa za kuhamasisha umoja wa kitaifa kupitia vijana
wa mkoa wote wa Singida, amewataka watanzania walionusurika na ugonjwa wa Corona
na wale waliopona kuendelea kuchukua tahadhari zinazoelekezwa na wataalamu na
Rais, ili kuepuka maambukizi mapya.
“Kwa wakristu
mkifatilia kitabu kile cha ‘Kutoka’ mtakumbuka namna Mungu alivyomuongoza Musa
katika kuwavusha wana wa Israeli kwenye bahari ya Shamu kwa kutumia ile fimbo…na
ndivyo baba yetu Magufuli anachokifanya kwa sasa,” alisema Ndahani huku akishangiliwa
Kupitia
maombi hayo ya shukrani, Sista wa Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu,
Jimbo Katoliki la Singida, Maria Subi, alisema anamshukuru Mungu kwa namna ya
kipekee hasa anavyojidhihirisha katikati ya kiongozi mkuu wa Tanzania Rais
Magufuli, kwa namna anavyoonesha hekima na utulivu mkubwa... wakati wote anaposhughulikia
suala la corona
“Kwa nguvu
yake Mwenyezi Mungu furaha na amani ya watanzania imeanza kurejea tena, na
tayari tumeanza kuungana na wageni mbalimbali kwa kuwakaribisha. Naamini sasa tutaendelea
kufanya kazi zetu kama kawaida na nchi itachangamka kama mwanzo, tunapaswa kumshukuru
Mungu” alisema Subi.
Post A Comment: