Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma akitoa onyo kwa shule na vyuo kuwaagiza wanafunzi kwenda na Spiriti,Malimao na Tangawizi pindi watakaporejea darasani Juni 1,2020
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amepiga marufuku vyuo na shule ambao wanawaagiza wanafunzi wao kwenda na spiriti, malimao na tangawizi badala yake wazingatie Muongozo uliotolewa na Wizara ya afya ju ya kujikinga na corona pindi watakapo fungua Juni Mosi.
Kemeo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Prof. Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kukemea vikali vyuo na shule hizo kuanza kuainisha vifaa mbalimbali vya wanafunzi kwenda navyo bila kuzingatia mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya.
Aidha Prof. Ndalichako amekemia uongozi wa taasisi za elimu kutumia Corona kama kitega uchumi kwa kuanza kuagiza wanafunzi kwenda na vitu ambavyo havipo kwenye mwongozo wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee Watoto .
Prof. amewaonya wanafunzi kuanza kudaiwa ada wakati walikuwa wameishalipa ada kabla ya kufunga shule, kwa hiyo walikwenda nyumbani kwa sababu kulikuwa na changamoto ya ugonjwa wa corona.
Pia Profesa Ndalichako ametaja mambo muhimu yaliyosisitizwa kwenye mwongozo huo wa Wizara ya Afya ni kuhakikisha kunakuwa na maeneo maalum ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na maeneo hayo kuwa ni mageiti, madarasa na kwenye mabweni.
“Katika mwongozo ambayo umesainiwa na Waziri wa Afya unasisitisa kunawa kwa maji tiririka na sabuni ndiyo iwe njia kuu na suala la vitakasa mikono liwe ni suala la hiari, lakini sio lazima, lakini kama vitakasa mikono vitakuwepo basi wazingatie vile vigezo ambavyo vimewekwa,” amesema Prof. Ndalichako.
Wizara imesisitiza na kushauri wazazi na walezi kuwapatia watoto wao barakoa ambazo zimeshonwa kwa kitambaa ambazo mwanafunzi anaweza akafua akapiga pasi.
Amesisitiza kuwa wanafunzi wanapoenda shuleni wazingatie umbali kati ya mtu na mtu, wajiepushe na misongamano iwe ni katika majadiliano, kwenye mabweni na wakati wa kula.
Post A Comment: