MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata ole Sanare ameagiza Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Charles Komba asimamishwe kazi mara moja kutokana na utoro kazini na kutohudhuria kikao cha Baraza la Madiwani kilichotakiwa kufanyika Mei 26, mwaka huu.
Sanare alitoa agizo hilo mwanzoni mwa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kilicholenga kujadili taarifa na majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19, jana.
Akiendesha kikao hicho, Sanare alitaka kujiridhisha iwapo wakuu wa
idara wote na vitengo wameshiriki kama ilivyokuwa imeelekezwa siku chache kabla ya kikao hicho, ndipo alibaini kutokuwepo ofisa huyo.
Alisema kibali alichokuwa ameomba kusafiri tangu siku ya kikao hicho, kilikuwa hakijapitishwa na
mkurugenzi wa halmashauri, huku akiwa hayupo kazini.
Alipoulizwa mkuu wake wa Idara ya Uhasibu kuhusu kutokuwepo kwake kazini, alikiri mtumishi huyo aliomba ruhusa, hakuruhusiwa na alitaarifiwa asiondoke.
Sanare alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Morogoro, Rehema Bwasi kumsimamisha kazi mara moja,
huku akimtaka pia kusimamisha mshahara wake hadi pale suala lake
litakapopatiwa ufumbuzi.
“Yaani nikitoka sasa hivi hapa uwe umemwandikia barua ya kumsimamisha kazi huko huko alipo kwa utoro wake, usimlipe mpaka jambo lake litakapopatiwa utatuzi,” alisema Sanare.
Post A Comment: