Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amezuia madereva wa malori ya mizigo kutoka Kenya kuingia nchini Tanzania badala yake mizigo hiyo ishushwe kwenye mpaka wa Sirari na kufaulishwa kwa magari yaliyopo upande wa Tanzania huku taratibu zote za kuendelea kupima ugonjwa wa corona zikiendelea .
Mh. Malima amesema kuwa uamuzi huo unatokana taarifa zinazotolewa kutoka nchi jirani ya Kenya zikidai kuwa maderava wanaotoka Tanzania kuingia Kenya wengi wao wana ugonjwa wa corona jambo ambalo alidai kuwa lina utata hivyo ni vema na wao pia madereva wao wasiingie nchini kupitia mpaka huo.
Amesema kuwa serikali ya Tanzania haina shida na maamuzi ya nchi ya Kenya kufunga mipaka yake kwavile nchi hiyo ni nchi huru yenye uwezo wa kufanya maamuzi yoyote juu ya mipaka yake.
"Kama wao wanawakataza kwenda kwao acheni msiende huko lakini pia sisi na Kenya ni ndugu wamoja,ni haki yao kufunga mipaka yao maana wao ni nchi inayojitegemea na sisi tunajitegemea,hakikisheni mnafanya shughuli zenu bila kuathiri chochote
"Tutaweka eneo Maalum ambalo tutakuwa tunabadilishia mizigo na bidhaa zetu zinazotoka kenya kuja Tanzania zichukuliwe hapo na zinazoenda kenya zichukuliwe hapo lengo nikuhakikisha shughuli zenu madereva zinaendelea na mnakuwa na amani hakutakuwa na kulalamika tena"RC Adam Malima

Post A Comment: