Mkuu wa Mkoa Iringa Ali Hapi amezindua rasmi mpango wa utoaji elimu kwa Mkoa wa Iringa utakaotekelezwa na Redcross katika Wilaya zote tatu za Mkoa wa Iringa.
Aidha amepokea vifaa kwa ajili utaoji elimu ikiwa ni pamoja na Magari 5 na vipeperushi 5000 na mabango 6000 kutoka kwa Rais wa Red Cross Tanzania, Ndg. David Mwakiposa Kihenzile. Katika hafla hiyo, RC Hapi aliambatana na Mkuu wa Wilaya Iringa Richard Kasesela kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Mganga Mkuu na viongozi mbalimbali wa Mkoa, Viongozi wa Redcross Mkoa na Voluntia kutoka Wilaya zote za Iringa.
Rais wa Red Cross Ndg Kihenzile ampongeza kazi inayofanywa na Mkoa wa Iringa na kuwashukuru wadhamini wa mradi huo ambao ni Belgium Redcross ) kwa kuona umuhimu wa kusaidia uelimishaji katika mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa amepongeza uongozi wa Redcross kwa kazi kubwa wanayofanya tangu waingie madarakani ambapo mabadliko makubwa yanaonekana na ameahidi Mkoa wake utaendelea kutoa ushirikiano kwa kadri iwezekanavyo.
Post A Comment: