NA HERI SHAABAN
RAIS John Magufuli ametoa shilingi Bilioni 2 kwa TARURA kwa ajili ya kutengeneza Barabara ya Barakuda Vingunguti kwa Kiwango cha lami.

Ujenzi rasmi wa barabara hiyo unatarajia kuanza Julai Mosi mwaka huu ambapo itajengwa chini ya usimamizi wa Tarura.

Akizungumza katika kikao cha halmashauri Kuu kata ya Vingunguti Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto alisema  fedha hizo zimetolewa na Rais kwa ajili ya kutatua kero ya muda mrefu.

"Ujenzi wa machinjio ya Vingunguti umegharimu sh, bilioni 12 mradi wa serikali umefikia hatua nzuri  kwa sasa  nijambo la kujipongeza wana Vingunguti pia Rais ameingiza Tarura fedha ya Barabara hiyo iloyokuwa kero ili ijengwe" aliema.

Meya Kumbilamoto ameipongeza serikali ya John Magufuli katika kufanikisha  usimamiaji miradi ya Maendeleo.

Alisema katika kufanikisha miradi ya Maendeleo serikali imeweza kufanikisha miradi mbali mbali ya Maendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi wa Tanzania ya viwanda.

Alisema mara baada kukamilika kwa  machinjio hayo ajira zitapatika kila siku manispaa ya Ilala imeshaweka taratibu.


Wakati huohuo alisema Halmashauri ya Ilala imetoa fidia shilingi milioni 500 kwa ajili ya kununua nyumba 15 ili eneo litumike kwa wafanyabiashara wa eneo hili ambapo wakati wowote nyumba hizo zitavunjwa mara baada fidia yao.

"Ujenzi wa machinjio hayo ya Vingunguti ni sehemu ya kiwanda  machinjio haya ya Kimataifa changamoto ilikuwa barabara wageni wakija ni aibu Serikali yetu imetoa fedha  sasa hivi kutakuwa Ulaya ndogo.

Alisema machinjio hayo yana sehemu za nyumba ya ibada ndani Msikiti na Kanisa kwa ajili ya waumini wake ambao wanafanya kazi katika machinjio hayo.

Mwisho
Share To:

Post A Comment: