Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge,akizungumza na wananchi wa kata ya Pahi wilayani Kondoa kuwahamasiha kutumia mfumo wa Stakabadhi ghala katika kuuuza zao la ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge,akisisitiza jambo kwa wananchi wa kata ya Pahi wilayani Kondoa wakati akiwahamasisha kutumia mfumo wa Stakabadhi ghala katika kuuuza zao la ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
Baadhi ya wakulima wa zao la Ufuta wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge,wakati akiwahimiza wananchi wa kata ya Pahi wilayani Kondoa kutumia mfumo wa Stakabadhi ghala katika kuuuza zao la ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
Mkuu wa wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota ,akizungumza na wananchi wa kata ya Pahi wilayani Kondoa kwa kuwahimiza kutumia mfumo wa Stakabadhi ghala katika kuuuza zao la ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kondoa Bw.Mustapha Semwaiko ,akizungumza na wananchi wa kata ya Pahi wilayani Kondoa kwa kuwahimiza kutumia mfumo wa Stakabadhi ghala katika kuuuza zao la ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
Meneja Ghala kutoka Kampuni ya Spendors Control Ltd,akitoa elimu kwa wananchi wa kata ya Pahi wilayani Kondoa jinsi ya kutumia mfumo wa Stakabadhi ghala katika kuuuza zao la ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge,akitoa maelezo kwa viongozi wa wilaya ya Kondoa alipofanya ziara ya kujionea mnada wa zao la ufuta kwa kutumia mfumo wa Stakabadhi ghala katika kuuuza zao la ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
.............................................................................
Na.Mwandishi wetu, Kondoa
Halmashauri za Mkoa wa Dodoma zimetakiwa kutumia mfumo wa Stakabadhi ghalani katika bidhaa ya ufuta ili kulinda maslai ya mkulima.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge akiwa katika ziara ya kikazi katika wilayani Kondoa kujionea mnada ulioendeshwa kwa ajili ya kuuza ufuta kwa kutumia Stakabadhi Ghala .
Dkt. Mahenge amesema kuwa kila uongozi wa halmashauri mkoani Dodoma unatakiwa kuhakikisha unadhibiti vema mfumo huu kufanya kazi ili kudhibiti ubora wa ufuta .
Dkt. Mahenge amesema kuwa vipimo vidhibitiwe ili mkulima kuwa na amani katika bidhaa yake kwamba imepita kwenye minzani ambayo ni sahihi.
Dkt. Mahenge amesema kuwa kunahaja ya kuongeza vituo vya ukusanyaji ufuta ili kumpunguzia mkulima umbali wa kusafirisha mazao yake.
Aidha Dkt.Mahenge amesema kuwa wafanya biashara wadogo ngazi ya Kijiji wanaweza kuuziana wenyewe mazao ili kuweza kujipatia fedha ya mahitaji muhimu kama pesa ya matibabu na yule aliyenunua lazima apitishe mazao hayo kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani.
“Kiwango cha kununua kwa mkulima kisiwe zaidi ya kilo 100 zaidi ya kilo 100 mtu anaweza kwenda kuuza katika mfumo rasmi wa stakabadhi ghalani”ameeleza Dkt. Mahenge.
Aidha Dkt. Mahenge ameema kuwa kuwa ufuta utakaokusanywa utapelekwa kwenye mfumo rasmi ili mkulima kupata stahiki zake ambapo mkulima atalipwa ndani ya siku 10 baada ya mnada.
“Natoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Dodoma kufungua benki akaunti ili kurahisisha malipo yenu katika ulipwaji “, ametoa rai Dkt. Mahenge.
Dkt. Mahenge amesema kila halmashauri mkoani humo kuendelea kufanya uhamasishaji na kutoa elimu kwa wananchi kuanzisha vyama vya ushirika na masoko ya ndani ya vijiji kwa lengo la kuwasogezea huduma wananchi wanao wahudumia.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota amesema kuwa mazao ya choroko,dengu, mbaazi na ufuta yatauzwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwa lengo la kumkomboa mkulima kufikia malengo yake ikiwa ni sehemu mojawapo ya kumtia moyo katika kwendeleza utendaji wake katika kilimo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa Pabui AMCOS Mzee Juma Hussein amesema kuwa wao kama chama cha ushirika wanajukumu kubwa la kutafuta masoko ili kuuza mazao hayo ya wakulima na kufanyikisha wakulima kupata hakizao bila kukandamizwa.
Akitoa neno la shukrani mmoja wa wananchi wa wilaya ya Kondoa amesema kuwa anashukuru kwaniaba ya wanaKondoa kuwa awali hawakuwa na elimu juu ya kutumia mfumo hu una sasa wanafarijika kikubwa ni kuendeleza uhamasishaji kwa wananchi ili kuweza kutumia mfumo huo kikamirifu.
Post A Comment: