Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi akizungumza wakati akitoa elimu katika semina ya siku mbili  inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga,
 Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi akizungumza wakati akitoa elimu katika semina ya siku mbili  inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga
 Programu Meneja wa Shirika la TEWOREC Halima Jabiri Saguti akisisitiza jambo jana wakati akitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wasaidizi wa kisheria Mkoani Tanga yaliyoendeshwa na Shirika hilo Jijini Tanga kwa kushirikisha wilaya zote za mkoa huo
 AFISA wa Tathimini na Ufuatiliaji wa Taasisi ya TEWOREC akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mashaka Mhando akitoa uzoefu wake wakati wa semina hiyo

 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia


HALMASHAURI ya Jiji la Tanga, imempongeza Rais John Magufuli, kwa hatua alizochukua kukabiliana na ugonjwa wa Corona nchini.

Sambamba na pongezi hizo, ugonjwa huo katika Jiji la Tanga unapungua kwa kasi kutokana na wananchi wengi kuchukua tahadhari zinazotolewa na Serikali pamoja na wataalamu wa afya.

Akizungumza kwenye semina ya siku mbili inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga, Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi alisema wananchi hawana budi kumpongeza Rais kutoka na kututoa hofu tangu alipogundulika mgonjwa mmoja hapa nchini.

Alisema kweli ugonjwa huo bado upo nchini na wananchi waendelee kuchukua tahadhari zote pamoja na kwamba maambukizi yanashuka kwa kasi kubwa Jijini hapa, lakini pia wanampongeza Rais kwa hatua alizochukua hadi ugonjwa unaendelea kupungua.

"Ugonjwa upo na Tanga pia upo, tuchukue hatua tunazoelekezwa na wataalamu wetu wa afya, lakini kwa kweli tunampongeza mheshimiwa Rais kwa kututia faraja tangu ugonjwa huu umeanza," alisema Maulidi.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walisema yametolewa wakati muafaka ambao shughuli za kiserikali nyingi zimeanza kufanyika baada ya mikusanyiko kuzuia hivyo itawasaidia kupata uelewa mkubwa wa ugonjwa huo na taadhari zake.

Awali akifungua mafunzo hayo Meneja wa Shirika la kutoa msaada wa kisheria mkoani Tanga (TAWOREC) Halima Saguti alisema lengo la kutoa mafunzo kwa Paralegal hao ni kutaka wanapotoa huduma kwa wananchi huko vijijini waweze kujiinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Alisema kazi za wasaidizi hao wa kisheria zimekuwa zikiendelea huko vijijini na hivyo kupewa elimu hiyo kutasaidia kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo kwa watu wengine.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: