NA HERI SHAABAN

MEYA wa halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amefanya ziara ya kikazi jimbo la Ukonga kuangalia maendeleo ya ujenzi   wa barabara hiyo na daraja la muda la watembea kwa miguu Ulongoni A.

Akizungumza katika ziara hiyo eneo la Ulongoni A Meya Kumbilamoto aliagiza mafundi wanaojenga kivuko hicho  kimalizike kwa wakati ili wananchi waweze kutumia.


"Wananchi wanapata shida kwa sasa wanapita katika maji naomba mkandarasi wa ujenzi huu angalieni wananchi wetu wanapata shida  kutokana na mawasiliano kukatika  kutokana na maji ya Mto Msimbazi ambayo yalivunja daraja la awali "alisema  Kumbilamoto.


Aidha alisema Mkandarasi huyo anayejenga daraja la muda ndio amepewa tenda ya kujenga barabara hiyo kuelekea Kinyerezi  pamoja na daraja la kudumu    mradi unaofadhiliwa na DMDP  .

Katika ziara hiyo ,Kumbilamoto ameongozana na msafara wake Katibu wa  Mbunge wa Jimbo la Ukonga  ,Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Gongolamboto  na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Wakati huo huo Meya Kumbilamoto amefanya ziara katika Zahanati ya Serikali ya Bangulo kuangalia maendeleo ya zahanati hiyo ambapo kwa  sasa imeshaanza  kazi ,changamoto kubwa ukosefu wa umeme Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wameshalipwa fedha na Halmashauri ya Ilala toka mwezi Marchi mwaka huu ila umeme bado kufika kwa wakati.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: