Majadiliano ya viongozi wa Serikali mkoa wa Arusha kwenye soko la Samunge jijini Arusha wakati ukarabati wa miundombinu ukiendelea leo |
Biashara zikiendelea mama akiwa na sufuria kichwani akipita katika ya eneo la Soko la Samunge kuendelea na kazi za Ujenzi wa taifa |
Wafanyabiashara wakisubiria kuhakiki maeneo yao kabla ya ujenzi kuanza |
Biashara zinaendelea huku wafanyabiashara wakingojea kupangiwa maeneo na Serikali kupitia Uongozi wao kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha. |
Serikali mkoani hapa imehamia kwenye soko la Samunge lililoungua mwishoni mwa wiki kwa lengo la kuhakikisha kila mfanyabiasha anapata eneo lake pamoja na kuona uwekaji sawa wa miundombinu na ugawaji wa maeneo ndani ya soko hilo.
Akiongea kwenye hadhara hiyo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alieambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa tokea Asubuhi ya Leo amesema kuwa atahakikisha kila mfanyabiashara aliekuwepo kwenye soko hilo anapata eneo la kufanyabiashara.
Alisema kuwa wapo watu wanaotaka kutumia nafasi hiyo kujipenyeza amewataka kukaambali kwani Serikali haitasita kuwachukulia hatua Kali za kisheria pamoja na wale wanaodhani huu Sasa ni wakati wa kufanya mzaha waache Mara moja kwani hayo ni maisha ya watu.
Amewatoa hofu wafanyabiashara hao na kuahidi Serikali kuwepo eneo hilo kwa siku nzima ya leo kuona kila alieunguliwa anapata eneo lake ili aanze ujenzi Mara moja ikiwemo na kufanyabiashara.
Amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuwepo kwenye eneo hilo na kusaidia kuona wafanyabiashara hao wakianza shughuli za kujipatia kipato kwani wanategemewa na kama tutachelewesha kumaliza familia zao zatakufa njaa ndio maana tupo hapa Leo nzima.
Kwa Upande wake Kaimu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Joseph Massawe ameendelea kuitaka Serikali kuhakikisha inamaliza kuweka miundombinu kwa haraka ili wafanyabiashara hao waanze kazi Mara moja
Nae Kamanda wa Kikosi Cha Zimamoto alisema kuwa miundombinu hiyo ya barabara itaanzia kusini na kaskazini na upande mashariki na magharibu kutakuwa na barabara ambayo itasaidia pindi litakapotokea tukio kama hilo kuwe na njia ya kupitika kuweza kuzima na kuokoa Mali kwa haraka tofauti na kipindi kilichopotia.
Awali kaimu kamanda wa Polisi mkoani hapa Koka Moita aliwatoa hofu wafanyabiashara hao na kuwaambia jeshi hilo litashuhulika na yeyote ambaye atabainika kuleta uvunjifu wa Amani katika eneo hilo na wataendelea kufuata maagizo ya mkuu wa mkoa hadi kuona kila moja anafanya kazi zake kwa usalama.
Post A Comment: