SHAURI dogo namba 5 la mwaka 2020 lililofikishwa katika mahakamani na mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe (Chadema) kupinga mchakato wa madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) kutoka kumung'oa katika nafasi yake limeondolewa mahakamani leo .
Akisoma hukumu ya kesi hiyo hakimu mkazi wa mahakama Iringa Aden Kanje alisema kuwa maombi yaliyofikishwa mahakamani hapo na mlalamikaji huyo Alex Kimbe ambae katika kesi yake hiyo alikuwa akitetewa na wakili Barnabans Nyalusi vifungu ambavyo vilitumika kufikisha maombi hayo vilikuwa vimekosewa .
Hakimu huyo alisema kuwa hoja za upande wa wakili wa serikali alidai kuwa hoja za mleta maombi mahakamani hapo hazikuwa zimezingatia vigevyo vya kisheria hivyo aliomba mahakama hiyo kutupilia mbali maombi hayo ya Kimbe kutokana na kutokidhi vigezo vya kisheria pia aliomba kupewa gharama alizozitumia katika kufanya utafiti juu ya shauri hilo kutoka kwa mleta maombi mahakamani hapo
Wakati upande wa wakili wa mleta maombi mahakamani hapo Barnabans Nyalusi aliomba mahakama hiyo kutoa zuio la kumng'oa meya huyo madarakakani kwa madai kuna taratibu ambazo zinapaswa kufanyika kabla ya kumwondoa meya huyo madarakani .
Pamoja na hoja nne ambazo zilitolewa na wakili wa serikali katika kupinga maombi hayo kusikilizwa na hoja zilizotolewa na wakili mlalamikaji juu ya kupinga hoja za wakili wa saerikali mahakama hiyo imelitazama suala hilo kisheria na kitaratibu za kimahakama na kuona hoja za upande wa wakili wa serikali zina mashiko na kuwa hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo la kuzuia kumng'oa meya madarakani .
Kwani imeona maombi yake yalitokana na hisia za mwombaji wa zuio hilo kuwa yawezekana yasingefanyika hivyo na kimsingi mahakama kifungu kilichotumiwa na mleta shauri hilo mahakamani kilikuwa na makosa ya kisheria .
Alisema kuwa kifungu namba 2(3) kilichotumiwa ni kifungu kinachosimamia masuala ya sheria na mahakama ( Judicature and Apllication of Laws ( JALA ) kuwa pamoja na kifungo namba 95 na 68 (E) vya sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai .
Kuwa mahakama hiyo haipati nguvu ya kimaamuzi katika shauri hilo hilo hivyo kwa msingi huo maombi hayo yamekosa nguvu za kisheria hivyo mahakama imelazimika kuyaondoa mahakamani hapo na rufaa ipo wazi ndani ya siku 45 kwa upande wowote ambao utakuwa haujaridhika na uamuzi huo wa mahakama kuwa Mahakama inaliondoa shauri hili kwa gharama za uendeshaji wa kesi kwa upande uliopoteza .
Akizungumza na wanahabari nje ya mahakama hiyo baada ya hukumu hiyo kutolewa wakili Nyalusi alisema kuwa anakubaliana na uamuzi wa mahakama na kuwa ambacho atakifanya ni kwenda kuziangalia hoja ambazo zimetolewa na mahakama katika hukumu hiyo ili kuona namna ya kurudi mahakamani hapo .
" Hakimu hajafuta kesi kwa kutumia vifungu ila amesema vifungu ambavyo sisi tumevitumia kuombea maombi yetu si sahihi yeye ametoa kifungu ambacho lazima tukakisome na kuona maana zipo kesi ambazo zimesikilizwa na mahakama kuu na kutumiwa kifungu hicho hicho alichokitoa yeye tunaamini tutakwenda kusoma na tutashauriana vizuri na hii sio mwisho " alisema wakili Nyalusi .
Hata hivyo alisema kuwa wao walikuwa wanazuia mchakato wa kumuondoa meya madarakani sio kuzuia meya kuondolewa kwa kuamini kuwa mchakato huo haukufuata sheria maana kanuni za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa zinaeleza wazi ili meya aondolewe kuna taratibu za kufuata ila hazikufuatwa na kwa kuwa kilichojadiliwa mahakamani si maombi yao ya msingi ila kilichojadiliwa na kutolewa maamuzi ni taratibu sio hoja zao .
Hata hivyo hivyo alisema kuwa hawezi kusema zaidi juu ya maamuzi ya mahakama ila wanakwenda kujipanga zaidi maana hoja zao za msingi mahakama hiyo haijaweza kuzigusia kabisa zaidi ya kutolea uamuzi taratibu wa za ufikishaji wa maombi hayo mahakamani hapo .
Kuhusu kuendelea kwa mchakato wa vikao vya kutaka kumwondoa meya madarakani alisema kuwa wao hawajui kwanini mchakato huo unaendelea kwani kimsingi kesi inapokuwepo mahakamani watu wenye hekima huwa wanasimamisha shughuli zote ila wanashangaa kuona mchakato ukiendelea kuitwishwa .
Shauri hilo la mstahiki meya Kimbe kwenda mahakamani kupinga mchakato huo wa kumwondoa lilifikishwa mahakamani hapo Machi 17 kabla ya jana Machi 27 kutolewa maamuzi na mahakama hiyo japo wakati mahakama meya huyo akiwa mahakamani hapo mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Himid Njovu ameitisha kikao cha dharua cha baraza la madiwani kitakachofanyika leo baada ya kikao kama hicho kilichokuwa na ajenda ya kumung'oa meya kushindwa kufanyika juzi kwa kukosa mahudhuria ya wajumbe 17 ambayo ni therufi mbili ya wajumbe 26 ambao walipaswa kufika katika kikao hicho na badala yake kufika wajumbe 15 pekee .
Kabla ya kuanza kwa kikao cha juzi ambacho kiliahirishwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Njovu alisema kuwa ili kikao hicho kiweze kuendelea kwa mujibu wa kanuni namba 9,2 kanuni ya kudumu ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa za 2015 zinaeleza kwamba akidi ya wajumbe wa mkutano maalum wa Manispaa hiyo itakuwa ni therufi mbili ya wajumbe wote na itahesabiwa wakati wa ufunguzi wa mkutano .
“ Kwa kanuni hiyo naomba ndugu mwenyekiti na CC (katibu wa kikao) wetu atuhesabie wajumbe waliopo katika mkutano huu na therufi mbili ya wajumbe wa mkutano huo na therufi mbili ya wajumbe 26 wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni wajumbe 17 na kama idadi hiyo itatimia basi mwenyekiti atafungua mkutano huo ili uendelee na kama idadi haitatimia basi mwenyekiti na baraza lake atatoa maamuzi atakayoona yanafaa” alisema Njovu na kukaa chini
Post A Comment: