WADAU wa maendeleo mkoani Arusha,wametoa ,misaada ya vitakasa mikono vyenye thamani ya shilingi milioni 3.9 kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.
Akikabidhi msaada huo jana kwa uongozi wa mkoa wa Arusha,Meneja wa kampuni ya Planet phamasetcal limited,Joseph Lekumok,amesema msaafa hio ni sehemu ya mchango kusaidia kukabiliana na ugonjwa wa Corona ambsolo ni janga la ulimwengu.
Akipokea msaada huo Katibu taaala sa mkoa wa Arusha,Richard Kwitega,amesema mkoa bado uauhitaji wa misaada mbalimbali ikiwemo vitakasa mikono kwa ajili ya kukinga wananchi fhifi ya maambukizi ugonjwa wa Corona.
Amewapongeza baadhi ya wadau wakiwemo benki ya CRDB na hifadhi za taifa,Tanapa,kwa misaada yao katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona,na akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kutoa misaada yao.
Kuhusu mkoa kutekeleza maelekezo ya kutenga maeneo maalumu ya wagonjwa wa Corona,kutoka kwenye nchi zenye ugonjwa huo,amesema tayari mkoa umeshatenga maeneo ya kutosha kwa ajilu ya wote watakaogundulika kuwa na maambukizi ya Corona.
Amesema wote watakaokutwa na maambukizi watawekwa kwenye maeneo hayo yaliyotengwa ambayo watakaa humo kwa muda wa siku 14,kwa gharama zao wakati wakipata matibabu mpaka wataalamu wa afya watakapoona afya zao zimetengemaa lengo ni kuzuia maambukizi kwa wengine.
Amesema hadi kufikia Marchi 24 mkoa ulikuwa haujapokea mgonjwa wa Corona,na serikali inaendelea kufuatilia taarifa kwenye maeneo yote ya mipakani na viwanja vya ndege ili kuwatambua na kuwadhibiti,wote wanaoingia nchini kama wana maambukizi ya Corona.
Post A Comment: