CHAMA cha wamiliki wa magari ya masafa marefu mkoa wa Arusha ,TABOA,Hakiboa pamoja na wasafirishaji wenza wameiunga serikali mkono katika swala la kupiga vita ugonjwa wa Corona pamoja na kutoa elimu ya kuchukuwa taadhari juu ya ugonjwa huo kwa kunua dawa ,mabomba ya kunyunyuzia dawa ,dawa za kunaiya mikono pamoja na ndoo 100 za kuwia mikono pamoja na kuzindua rasmi zoezi la upigaji dawa kwa vyombovyote vya usafirishaji vilivyopo mkoani hapa
Akizungumza wakati wa kukabithi vifaa hivyo katibu wa Taboa ambaye pia ni mmiliki wa mabasi ya abiria yajulikanayo kwa jina la Kimotco Benedict John Mberesero (ben Kimotco) alisema kuwa wameamua kuunga mkono serikali katika swala zima la kupiga vita ugonjwa huu wa Corona ambao ni gonjwa linalotikisa dunia nzima kwa sasa kwa kununua vifaa ambavyo vinaweza kuwakinga wananachi juu ya ugonjwa huu .
Alisema kuwa vifaa hivi walivyonunua vinagarimu kiasi cha shilingi milioni 13 ya kitanzania na watavisambaza katika maeneo yote ya mkoa wa arusha ambapo alaibainisha kuwa pia watahakikisha vyombo vyote vya usafiri vinapigwa dawa kwa ajili ya kuzuia ugonjwa huu ,huku akibainisha kuwa zoezi hili limeanza ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha na wanatarajia kulifanya katika halmashauri zote za mkoa wa Arusha .
“hatutakubali kuona mtu anakufa kutokana na ugonjwa huu kitu tutakacho kifanya tutatoa elimu kwa abiria wetu ,wananchi wote wanaoingia standi na kupanda magari yetu juu ya kuchukuwa taadhari ya ugonjwa huu ,na nisema tu swala hili tunaomba tuwaambie abiria wasikatae kunawa mikono pale tunapo waambia wanawe ,kwani wakifanya hivyo watakuwa wanavunja sheria na iwapo mtu akivunja sheria tutamchukulia hatua kali maana atakuwa atutakii mema “alisema Benedict
Akizindua zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro aliwapongeza viongozi hawa kwa kuunga serikali mkono wa kupiga vita ugonjwa huu na kubainisha kuwa ugonjwa huu ni mbaya hivyo ni vyema kila mwananchi kuchukuwa taathari juu ya ugonjwa huu ,aidha aliwataka wananchi kufuata maagizo yote ambayo wanapewa na viaongozi wa afya juu ya njia za kujikinga na ugonjwa huu.
Aliwataka wananchi kuondoa taaruki ,kutotishana bali waendelee kuchukuwa taathari huku akiwasihi kila mwananchi kuchukuwa taathari katika eneo lake na kuendelea kusikiliza miongozo inayotolewa na wataalam wa afya ,aliwasihi wananchi kutoleta mizaha wala kejeli katika swalahili kwani ni swala linalohusu maisha ya watu.
“kunatabia imezuka ya watu wenyemaduka wanaouza sanitizer kupandisha bei napenda niwaambie wananchi kile kidogo kinauzwa elfu tatu ukienda maahali ukakuta kinauzwa zaidi nipigie simu ,naniwaambie wauzaji msipandishe bei tukibaini mmepandisha bei hatu kali zakisheria tutawachukulia ,naniwasisitize wananchi tuzingatie usafi ugonjwa huu ni mbaya na unaua hivyo tujitaidi sana kuwa wasafi ili ugonjwa huu usitumalize”alibainisha Gabriel
Nae Mrakibu mwandamizi wa polisi Almachius Muchunguzi aliwataka wananchi wa mkoa wa Arusha kutii sheria bila shuruti ili kuepuka kuambukizwa ugonjwa huu ,
‘’iwapo umeambiwa usibebe abiria zaidi ya ukabeba apo utakuwa unavunja sheria na sisi kama jeshi la polisi atutakuvumilia,tukikwambia msikae kwenye mikusanyiko tukikukuta atutakuvumilia kwakweli hatua kali tutakuchukulia ,tukikwambia kaandani ukatoka utakuwa unavunja sheria na sisi atutakuvumilia ,ukileta maneno ya kizushi hatuta kuvumilia hivyo ni wasihi tu wananchi wa mkoa wa Arusha mtii sheria bila shuruti ili tuweze kujikinga na ugonjwa huu “alibainisha Muchunguzi
Post A Comment: