Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kushoto) akimkabidhi madawati Mwakilishi wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Puma,  Mwalimu Amani Kipandwa katika hafla iliyofanyika juzi. Wa pili kushoto anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi na kulia ni Diwani wa Kata ya Ikungi, Abel Nkuhi.
Wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo ya kupokea madawati.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Justice Kijazi 
akitoa taarifa fupi wakati wa hafla ya kukabidhi 
madawati hayo.
Makabidhiano ya madawati hayo yakiendelea.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ikungi, Orda Phabiani akizungumza.
Wanafunzi wakiwa katika hafla hiyo ya kupokea madawati.
Na Dotto Mwaibale, Singida
HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida 
imetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kutengene
za  madawati 1600 na kuhakikisha wanafunzi wote 
walioanza kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda 
shuleni na wanakaa kwenye viti.
Madawati hayo yamepatikana kutoka halmashauri hiyo 
na kuungwa mkono na wadau wa maendeleo pamoja na 
wabunge Elibariki Kingu na Miraji Mtaturu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo 
akizungumza  wakati akigawa madawati hayo 
alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, 
Justice Kijazi na watendaji wake kwa kazi hiyo kubwa 
walioifanya ya kutengeneza madawati hayo.
"Kwa nchi nzima halmashauri yetu imekuwa ya 78 kati 
halmashauri 195 zilizopo ni jambo la kujivunia na naamini 
kabisa ipo siku na sisi tutashika 
nafasi ya kwanza" alisema Mpogolo.
Mpogolo alisema wanafunzi wote 4, 517 waliochaguliwa 
kuanza kidato cha kwanza watakwenda shuleni na 
watakaa kwenye viti.
Alisema wadau wa maendeleo waliochangia ununuzi 
wa madawati hayo hawakufikiria familia zao bali 
waliwafikiria wanafunzi hao kwani lengo la halmashauri 
hiyo ni kuhakikisha madawati yote 3900 yanapatikana
 na kuwa watoto hao wote wanafika chuo kikuu.
Mpogolo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Magufuli 
kwa kuipa wilaya hiyo sh.1.3 Bilioni kwa ajili ya 
kugharamia  elimu pasipo malipo na sh.400 milioni 
za kugharamia ujenzi wa miundo mbinu.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Justice Kijazi 
akitoa taarifa fupi wakati wa hafla ya kukabidhi 
madawati hayo alisema fedha za kununua madawati 
hayo zilitoka katika mapato ya ndani na kuchangiwa 
na wadau wa maendeleo ambapo Benki ya NMB ilitoa 
viti 100 na meza, Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) 
sh. milioni 24 pamoja na wabunge wa Jimbo la Singida 
Mashariki na Magharibi ambao kila mmoja alitoa 
sh. milioni tano.
Alisema hatua hiyo waliifikia kufuatia ongezeko 
kubwa la  ufaulu wa watoto na kuhakikisha wote 
wanakwenda  shuleni na kuwa na viti vya kukalia.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: