Mkuu wa wilaya ya Chunya Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na wananchi wa kata ya Sangambi Chunya
Na Esther Macha Chunya
WANACHI wa Kata ya Sangambi tarafa ya Kiwanja Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamejitolea kujenga shule ya sekondari itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni m ili kuwaondolea adha wanafunzi ya kutembea umbali mrefu wa kilometa ishirini na saba hadi arobaini kwenda shule ya sekondari Kiwanja.
Awali akisoma taarifa kwa mkuu wa Wilaya wakati wa mkutano wa hadhara , afisa mtendaji Kata ya Sangambi Ntundu Chapa alisema mpaka sasa wamefanikiwa kujenga vyoo matoto kumi na mbili, madarasa mawili,maabara na jengo la utawala.
Kutokana na kadhia hiyo ya kutembea umbali mrefu baadhi ya wanafunzi wameacha shule na wengine kupata mimba za utotoni pia waliofanikiwa kumaliza matokeo yao yamekuwa si mazuri ambayo hayawawezeshi kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiingia gharama za kuwapangishia vyumba watoto wao lakini kutokana na kukosekana usimamizi wa karibu watoto wengi hawazingatii masomo kutokana umri mdogo na wengine wamekuwa wakiolewa.
Diwani wa Kata ya Sangambi Junjulu Mhewa katika kuwapa moyo wananchi alichangia zaidi ya shilingi milioni kumi katika ujenzi huo.
Mtendaji alisema Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alichangia mabati yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya , Bosco Mwanginde alisema
Halmashauri ya Wilaya Chunya imechangia shilingi milioni kumi na tano.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Chunya Cathbeth Mwinuka alisema Halmashauri itafanya kila namna ya kuongeza pesa ili shule iweze kusajiliwa kabla ya mwezi mwaka huu.
Afisa Elimu sekondari ,Hebeli Kibona alisema wananchi waongeze kasi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na maktaba,maabara pia nyumba za walimu.
Malongo Hasotte ni Mwenyekiti wa ujenzi mbali ya kuwapongeza wananchi na wadau mbalimbali kushirikiana ili kuyamalizia ujenzi kwa wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhandisi Maryprisca Mahundi alisema wananchi na wadau wajitokeze ili kuhakilisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaanza masomo kabla ya mwezi machi mwaka huu.
Mahundi alisema ili shule hiyo isajiliwe ni vema wananchi wakajielekeza kukamilisha maabara na majengo mengine.
Singa Duwila ni mmoja wa wananchi wa Kata ya Sangambi alisema Kata ina shule sita za msingi ambazo zina mlundikano wa wanafunzi madarasani hivyo pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari serikali izisajili shule shikizi katika Kata yao ili watoto wasitembee umbali mrefu.
Hata hivyo aliwaomba wazazi washirikiane katika ujenzi wa shule hiyo badala ya kuitegemea shule ya Kata nyingine.
Zaidi ya wanafunzi mia moja arobaini waliofaulu mwaka jana hivi sasa wanasoma shule ya sekondari ya Kiwanja.
Post A Comment: