Na Heri Shaaban
TAASISI ya amani Islamic Foundation yampongeza Rais John Magufuli kwa utendaji kazi wake na kusimamia amani ya nchi.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Taasisi ya amani ya Tanzania Islamic Foundation Sadiki Godigodi, wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mazuri yaliyofanywa na Rais wa awamu ya tano John Magufuli ikiwemo kudumisha amani na mshikamano kwa watanzania.
" Taasisi yetu kwa kushirikiana na viongozi wa dini mbalimbali tunachukua fursa hii ya kumpongeza juhudi za serikali ya Rais Magufuli kudumisha amani pia inawaonya watu wasitoe taarifa za uzushi za kutekwa watu bila kufatilia katika vyombo vya usalama" aliema Sadiki.
Sadiki aliema nchi yetu inaongozwa na sheria unapokuwa una shaka na jambo zipo mamlaka zimeundwa kwa ajili ya kufatilia usitoe taarifa ambazo ujazifanyia utafiti kwani vitendo hivyo vya uzushi havijengi umoja bali vinatengeneza dhana hasi miongoni mwetu kutoaminiana.
Said alisema tulizaliwa Tanzania tutazikwa Tanzania hivyo kila mmoja jukumu lake kubwa kulinda amani vizazi vyetu visihukumiwe kwa mambo yanayofanywa sasa kimsingi yataathiri maisha yao baadae.
Katika hatua nyingine wamempongeza Rais kwa hotuba nzuri aliyotoa hivi karibuni Zanzibar wakati wa madhimisho ya miaka 56 ya Muungano.
Aliwataka watanzania kudumisha amani nchi yoyote ikikosa amani akuna maendeleo kama kuna matatizo aliwataka watanzania mutumia njia za kutatua changamoto bila kuathiri amani, upendo na mshikamano.
MWISHO
Post A Comment: