Na John Walter-Manyara

Naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Juliana Shonza leo Jumatatu Januari 20-2020 akizungumza na wadau wa Sanaa mjini Babati katika mkoa wa Manyara,amewashauri wasanii hao kutumia zaidi Mitandao ya kijamii ili kutangaza kazi zao.

Aidha Naibu Waziri amewataka Wasanii hao kukumbuka kujiendeleza kielimu ili wafanye sanaa kisomi.

Pamoja na hayo,Mheshimiwa Naibu waziri amezichukua baadhi ya kazi za Wasanii kwa ajili ya kuzisikiliza na hatimaye kutafuta namna ya kuwasaidia kuzisambaza kwenye vituo vya Runinga.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: