Na Imma Masimba ,Mbuguni
Mbunge wa
Arumeru Mashariki Dr.John Pallangyo
ametoa msaada wa vyerehani 20 kwa wahitimu wa chuo cha Ufundi cha Next life
kilichopo kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru ili kuwawesha wahitimu hao kujiajiri
baada ya kumaliza masomo ili kujipatia kipato na kujiendeleza kiuchumi.
Akizungumza
katika mahafali ya chuo hicho ,Mbunge huyo amesema kuwa vijana ni nguvu kazi ya
taifa hivyo hawapaswi kukaa mitaani kusubiri kuajiriwa bali wanapaswa kuwa na
uthubutu wa kujiajiri hivyo vyerehani hivyo vitawawezesha kujiajiri.
Dr.John
amesema kuwa ataendelea kuwaunga mkono
vijana wenye nia ya kujikwamua kiuchumi
na kuchangia katika kufikia katika uchumi wa kati na uchumi wa viwanda
kama ilivyo adhma ya serikali ya awamu ya tano.
Aidha
amewataka vijana kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia
nidhamu na uadilifu ili waweze kutimiza malengo yao na kufanikisha ndoto zao.
Anaeleza
kuwa ataendelea kushirikiana na vijana
katika Wilaya hiyo katika masuala ya kimaendeleo pamoja na kuwaunga
mkono ili waweze kufanikiwa na kuchangia maendeleo katika familia,jamii na
taifa.
Post A Comment: