Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Zaidi ya ekari 3000 zimesimamisha
uzalishaji wa shayiri kutokana na wanunuzi wakubwa wa ngano inayozalishwa kata
ya Monduli juu kusitisha ghafla mkataba wa kununua mazao yao.
Wakulima wakizungumza katika kikao chao
,wamesema kuwa kusitishwa kwa mkataba wa kampuni ya mnunuzi kutawaathiri
wakulima kwani hawana mazao mbadala ya kuotesha kutoka na msimu wa mazao
mengine kupita jambo ambalo litawasababishia hasara.
Aidha Wakulima hao Loretu Leyan na Moloimet Sane wameshangazwa
na kitendo cha mnunuzi huyo kuvunja mkataba na wakulima licha ya kuwa mnunuzi
mzuri kwa miaka 20 ilitopita na sasa wakulima hawana mbadala.
Hata hivyo wakulima hao Langoi Katibu
wameiomba serikali iangalie ie namna mbadala ya kununua mazao yao
ili kuendeleza kilimo cha shayiri na kuwawezesha wakulima.kupata kipato.
Mwenyekiti wa Wakulima hao Sokoine
Leyan amesema.kuwa kusimama kwa uzalishaji
wa shayiri kutaathiri kipato cha wakulima na kupelelea kuzorota kwa maendeleo
hivyo ameiomba serikali ichukue hatua ili kuwanusuru wakulima.
Afisa Ushirika wa wilaya ya Monduli
Ester Tarimo amesema kuwa wakulima wa wilaya za jirani za karatu na mbulu pia wameathirika
na mnunuzi huyo kuvunja mkataba.
Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Monduli
Salimu Omar , amesema kuwa wamefika na kusikiliza kero za wakulima hao na
kuahaidi kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuleta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Hata
hivyo Wanunuzi hao ambao ni Maafisa wa Kampuni ya Bia ya TBL ,walifika
kuzungumza na viongozi katika kikao cha ndani ambacho hawakutaka
waandishi wa habari waingie na pia baada ya kumaliza kikao hawakutoa
ushirikiano wowote kwa wanahabari kwa maana ya kutokua tayari kuongea.
Post A Comment: