Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula kulia akimkabidhi katibu mkuu wa CCM Taifa Dkt Bashiru Ally hati ya shukrani kwa mchango wake katika chuo cha vijana Ihemi

Viongozi mbali mbali wakiwa katika ufunguzi wa chuo cha vijana Ihemi
Katibu mkuu wa CCM Taifa Dkt Bashiru Ally katikati na MNEC Taifa Salim Abri Asas kulia wakimhoji binti fundi kushona chuo cha vijana Ihemi
.......
KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi ( CCM) Taifa Dkt Bashiru Ally ameutenga rasmi uongozi wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) katika bodi ya vyuo vya UVCCM baada ya kuteua bodi ya muda ya watu 9 itakayosimamia chuo hicho ikiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa huku mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa anayetoka mkoa wa Iringa Salim Asas akiingizwa kuunda bodi hiyo .
Akitangaza bodi hiyo itakayosimamia chuo hicho jana baada ya uzinduzi wa chuo hicho ulioongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Philip Mangula alisema kuwa lazima CCm kujenga wanachama wenye moyo wa kukuza moyo wa kujitolea kwani alisema chuo hicho hadi sasa kimejengwa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 800 na kuna watu ambao walijitolea kwa kulala katika ujenzi wa chuo hicho na kushiriki shughuli mbali mbali kwa kujitolea na bila wao chuo hicho kisingekuwepo .
" Ili kuanza kusimamia vizuri na kwa sababu hakujawa na utaratibu ambao umepitishwa kamati kuu wa kuendesha vyuo hivyo ambavyo vinafufuliwa chuo cha Ihemi na vingine natangaza bodi ya muda ya kushauri namna ya kuendesha na kusimamia vyuo hivyo wakati utaratibu wa kamati kuu unaandaliwa natangaza vyeo vya watakaosimamia bodi hiyo si kwa majina " alisema Dkt Bashiru
Kuwa atakayekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa atakuwa mwenyekiti wa bodi ya ushauri ,atasaidiwa na atakayekuwa mkuu wa chuo ndie atakuwa katibu wa bodi hiyo na kwa kuwa bado hajateuliwa basi katibu wa CCM mkoa wa Iringa atakaimu nafasi hiyo hadi pale nafasi hiyo itakapojazwa .
wajumbe wengine ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda yeye atawakilisha kamati kuu katika bodi hiyo na anaanza mara moja ,mjumbe mwingine ni MNEC wa Iringa hata akiondoka yeye mwanachama atakayekuwa MNEC wa Iringa ndio atakayeshika nafasi hiyo , makatibu wa jumuiya za CCM mkoa na katika hilo watachaguliwa watu kwa uwezo na kama hawatatosha kwa sifa basi wataletwa watakaotosha .
Pia mlezi wa jumuiya ya vijana Taifa ,idara ya itikadi na uenezi itaweka pia mjumbe wake wakati makao makuu ya umoja wa vijana itafanya kazi ya kuratibu ,kuweka mikakati na kupitisha na malengo makuu kwa sababu wao pia wana vyuo vingine .
" Tunataka mkoa wa Iringa ushiriki vizuri na uongozi wake kutusaidia kuendesha chuo hiki na wote hao watakuwa chini ya ofisi yangu mimi katibu mkuu bodi hii itaanza kazi kuanzia leo hadi hapo kamati kuu itakapoweka bodi ya kudumu "
Dkt Bashiru alisema ili kuanza kusimamia vizuri vyuo vya UVCCM ambavyo vinafufuliwa kama Ihemi na Kibaha bodi hiyo itasaidia kuwashauri vijana wanaopata mafunzo katika vyuo hivyo na kuwasaidia kuacha kufikilia kuajiriwa.
“Natangaza bodi ya muda ya kushauri namna ya kuendesha vyuo hivyo wakati utaratibu wa kamati kuu unaandaliwa bodi hiyo itaundwa na watu wafuatao kwa vyeo sio majina, Mwenyekiti wa mkoa wa Iringa ambaye atakuwa ndio mwenyekiti wa bodi ya vyuo hivyo,atasaidiwa na atakayekuwa mkuu wa chuo na atashika nafasi ya katibu wa bodi,wajumbe wengine ni mlezi wa chama atawakilisha kamati kuu ya bodi hiyo”.
Awali akizindua majengo na miradi ya maendeleo ya chuo cha mafunzo Ihemi Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula aliwataka vijana kufuta fikra za kufikiria kuajiliwa badala yake wafikirie kujiajiri.
“mnapokuja kwenye mafunzo hapa chuoni nataka mfute kabisa mawazo ya tunajifunza ili tukaajiriwe,hapa sehemu ya mafunzo ni kubadilisha fikra na mitizamo ya kwamba kusoma ni kuajiriwa”alisema
Mangula alisema kuwa vijana wabadili mitizamo ya kusoma ni kuajiriwa wengi wasome wakijua watajitegemea na chuoni hapo watafundishwa namna ya kujiajiri kwani ajira kubwa ni kilimo.
Kwa upande wake Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa Mizengo Pinda alisema moja ya malengo ya chuo hicho ni kujenga hisia ndani ya vijana juu ya siasa ya nchi hii kwa maslah ya watanzania.
Alisema ni muhimu vijana kutambua uzalendo ni kitu gani hivyo unapoanza mafunzo ni muhimu kujikita katika siasa na itikadi ili waweze kujua taifa linataka nini kwa upande wa chama.
“Nimependezwa kuona chuo cha mafunzo ihemi kimekuwa ni kituo cha kuamsha hali na fikra mpya kwa vijana kisiasa na kimaendeleo,mna hekali 1963 yatatumika katika majengo lakini vilevile zitatumika katika kutoa mafunzo katika uzalishaji,kuna vitalu nyumba ufugaji wa nyuki na kilimo kwa ujumla”alisema
Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ajira na Vijana Antony Mavunde alisema vijana zaidi ya 200 katika chuo hicho walifundishwa kilimo kupitia kitalu nyumba na vijana 60,walifundishwa kupinda vyuma na kupitisha neti.
“Lengo lilikuwa ni baada ya muda mfupi tuwe na uwezo wa kuwatoa vijana wengi zaidi kutengeneza green house badala ya kuagiza nje ya nchi kama ilivyo sasa”alisema Mavunde
Waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Wilima Lukuvi alisema kuwa chuo hicho kimetengenezwa vizuri na wanahakika chuo hicho kiktakuwa mkombozi na kumshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kutoa kibali cha kuanzisha chuo hicho ambacho ni msaada mkubwa kwa vijana kwani kilipoanza kilikuwa na malengo kama hayo ila hayakutimia .
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema wakati wa ukombozi kazi kubwa ya chama ni hamasa,lakini baada ya uhuru siasa imebadilika imekuwa sayansi ni wakati sasa vijana wapate kufundishwa namana ya kujenga hoja na kupigania chama na kukilinda.
Christpher Ole sendeka Mkuu wa mkoa wa Njombe alisema anaipongeza CCM kwa kuyafufua mawazo ya Mhasisi wa taifa Julius Nyerere Kwa vitendo kwa kukifufua chuo hicho cha CCM.
“Huwezi kuwa na chama mazubuti chama makini bila kuwa na mahali pa kuwapika viongozi wake,chuo cha Ihemi kitaipa CCm nguvu mpya itakayoendana na kasi ya Rais wa Jamuhuli wa Tanzania Rais John Magufuli”alisema
Chuo cha Ihemi ni chuo cha kihistoria ambapo kwa muda mrefu kilisimama kutokana na changamoto mbalimbali,ambapo leo kimefufuliwa upya na kitakuwa na miradi 21 ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu kiasi cha 24 bilion na kinatarajia kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 14000.
" Wakati wa wa uongozi wangu nilipotembelea Ihemi na kukuta hali mbaya ya chuo wa kwanza kumpigia simu alikuwa Dkt Bashiru na wengi wanafikiri mimi nimekuwa tu kiongozi mimi ni zao la Dkt Bashiru hivyo najivunia chuo hiki kuanza leo "
Huku Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Mwl Raymond Mwangwala na mwenyekiti wake Taifa Kheri James nao wakitumia jukwaa hilo kujipongeza kwa kuanza kwa chuo hicho kuwa na jitihada zao na wanapaswa kujipongeza wenyewe kwa kazi hiyo kuwa .
Mwangwala alisema chuo hicho kinataraji kuwa na miradi zaidi ya 21 na kuwa hadi sasa chuo cha kushona sare mbali mbali kimeanza kwa msaada mkubwa wa MNEC Iringa Salim Asas aliyejitolea kujenga jengo la chuo hicho na zaidi ya shilingi milioni 800 zimetumika hadi sasa kati ya kiasi cha shilingi bilioni 22 zinazotarajiwa kutumika kujenga miradi yote chuoni hapo .
Post A Comment: