Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) jijini Dar es salaam leo kuhusu kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda linalotarajiwa kufunguliwa kesho na Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ukumbi wa Julius Nyerere.
Na Avila Kakingo Globu ya Jamii
WAFANYABIASHARA zaidi ya 1683 wanatarajiwa kihudhuria katika kongamano la kibiashara la nchi ya nchi mbili, Tanzania na Uganda litakalofanyka katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa wafanyabiashara zaidi ya 1056 wa Tanzania na wauganda 426 utafunguliwa kesho Septemba 6, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli wakishirikiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Waziri wa biashara na Viwanda Innoncent Bashungwa amesema kuwa maandalizi ya kufanyika kongamano la biashara kati ya nchi hizi mbili Tanzania na Uganda yamekamilika na hivi sasa tunapokea wafanyabiashara kutoka nchini uganda kwaajili ya kesho mapema saa tatu asubuhi kongamano hilo lifunguliwe na marais wetu wa Tanzania na Uganda.
Hata hivyo Waziri Bashungwa amesema kuwa wafanyabiashara hapa mchini wajiandae vyema katika kubadilishana uzoefu wa masuala ya biashara na wafanyabiashara wa Uganda ili kuunganisha dunia pamoja.
Amesema kuwa wafanyabiashara wa hapa nchini pamoja na taasisi mbalimbali za serikali watahudhulia mkutano huo ili kujadili sera na vikwazo vya kiuchumi na kibiashara katika nchi hizo mbili ili waweze kutatua na kufanya biashara bila vikwazo vigumu vya kibiashar
Post A Comment: