MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Kata ya Tangasisi wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake ya kawaida kufuatilia utekelezaji wa ilani ya CCM na kupata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi ambayo inafanyika mkoa mzima kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Diwani wa Kata ya Tangasisi Mohamed Haniu 
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo 
Diwani wa Kata ya Tangasisi (CUF) Mohamed Haniu akizungumza wakati wa ziara hiyo


 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella ambaye hayupo pichani wakati akizungumza nao
 Sehemu ya wakazi wa Kata ya Tangasisi  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga
 Sehemu ya wakazi wa Kata ya Tangasisi  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ameagiza walimu wanaofundisha Twisheni wafanya kazi hiyo nje ya majengo ya shule na nje ya muda wa kazi ili watoto watumie muda mwingi zaidi kusoma na kufundishwa.

Shigella aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwakidila wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake ya kawaida kufuatilia utekelezaji wa ilani ya CCM na kupata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi ambayo inafanyika mkoa mzima.

Alisema kwani walimu hao wanalipwa mshahara na serikali hivyo lazima wahakikishe wanatimiza majukumu yao ipasavyo kuwa kuwapatia elimu bora wanafunzi ambayo itakuwa chachu ya mafanikio kwao.

“Nimekuja hapa lakini nimesikia kuna baadhi ya watu wanalalamika juu ya twisheni, nimeelekeza kama kuna mwalimu anataka kufanya twisheni afanya nje ya majengo ya serikali na nje ya muda wa kazi”Alisemaq RC Shigella.

“Kwani lazima watoto wetu watumie muda mwingi zaidi kusoma na kufundishwa na walimu ambao wanalipwa mishahara na serikali wanapokuwa darasani muda wa masomo”Alisema RC Shigella

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba serikali itaendelea kuboresha mazingira ya watoto kusoma na kuendelea kupeleka walimu ikiwemo kutatua changamoto za walimu ili wafundishe kwenye mazingira mazuri na hatimaye waweze kupata wataalamu wengi zaidi.

Alieleza kwamba kupitia elimu watakuwa na watalaamu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, maji,afya na miundombinu na ndio maana serikali ya awamu ya tano imewekeza sana kwenye suala la elimu kuona watoto wanapata fursa hiyo muhimu.

Alisema pia serikali imeendelea kuleta fedha kwa ajili ya kukamilisha miundombinu kwenye shule mbalimbali huku akisifu juhudi zinazofanywa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kwa kuwasaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kwenye Jiji la Tanga.

“Waziri Ummy ni mwenzetu wana mwakidila kwa kutambua mchango ya shule yetu alikwenda kuongeza na ubalozi wa Japani na kusaidia madarasa sita hivyo hatuna budi kumshukuru kwa kazi nzuri ni Mbunge wa mkoa wa Tanga angeweza hayo madarasa kupelekea wilaya nyengine na ndio maana akaona aje kusaidia jitihada za wananchi kwenye eneo hilo”Alisema RC Shigella.

Hata hivyo alisema kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Waziri Ummy wanamshukuru huku akiwataka kuendelea kumuombea dua ili aweze kuendelea kutimiza majukumu yake.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: