Mikidadi Swalehe ni mkuu wa kitengo cha uhifadhi wa mabaki ya vyanzo vya mionzi ,katika Tume ya nguvu za Atomic (TAEC)Nchini ambaye pia ni mratibu wa mkutano huo unaoendelea Jijini Arusha,akizungumza na waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus.
Mkutano wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi unaofanyika Jijini Arusha.
Washiriki mbalimbali wa mkutano wa siku,tano wa majadiliano kama wanavyoonekana katika picha pamoja na uwakikishi wa mataifa waliyotoka.
Mwakilishi wa Shirika la Nguvu za Atomiki,Duniani,David  Bannet  David  Bannet  akitoa salamu ya shirika hilo ambalo ni mwangalizi wa Kimataifa wa masuala ya matumizi ya teknolojia ya Nyuklia
Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali kama inavyoonekana katika meza zao waliohudhuria mkutano wa siku tano unaoendelea Jijini Arusha katika hotel ya Corido Spring Jijini Arusha.
Mkutano wa majadiliano ukiendelea katika Hoteli ya Corido Spring Jijini Arusha ambapo TAEC ndiyo mwenyeji wa mkutano huo.
Mkutano wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi unaofanyika Jijini Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mkutano wa Kimataifa kwaajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha usalama katika kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi ,unaendelea Jijini Arusha na kukutanisha wataalam wa teknolojia ya nyuklia ,katika kujadili changamoto za usalama wakati wa uhifadhi wa mabaki hayo,ili kuepusha madhara kwa binadamu  na mazingira

Mikidadi Swalehe ni mkuu wa kitengo cha uhifadhi wa mabaki ya vyanzo vya mionzi ,katika Tume ya nguvu za Atomic (TAEC)Nchini,amesema kuwa mkutano huo umehudhuriwa na wanachama 30 ,kutoka nchi 21 duniani,ambapo umelenga katika kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti vyanzo vilivyomaliza muda wake lakini bado vinatoa mionzi.

 Mikidadi amesema jukumu la kusimamia usalama linahitaji nchi zote duniani ,kuhakikisha kwamba, vyanzo vyote vya mionzi vinakuwa katika mikono salama,ili kuepuka madhara mbalimbali ikiwemo kutumika kwa vyanzo hivyo katika masuala ya ugaidi.

Amesema kuwa vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi vinahitajika kuhifadhiwa mahali salama  palipo na ulinzi maalum,kwani hali hiyo itasaidia kuepusha vyanzo hivyo kuzagaa na kusababisha madhara mbalimbali kwa binadamu,na mazingira ,amesema TAEC inalo jengo maalumu kwaajili ya kuhifadhia vifaa hivyo vilivyomaliza matumizi yake.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA)  David  Bannet  akitoa salamu ya shirika hilo ambalo ni mwangalizi wa Kimataifa wa masuala ya matumizi ya teknolojia ya Nyuklia ,aliishukur Tanzania hususani TAEC kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Aidha amesisitiza kuwa  IAEA  itaendelea kushirikiana na nchi wanachama kuhakikisha kuwa teknolojia ya nyuklia itatumika kwa matumizi  salama ili isiathiri binadamu wa vizazi vilivyopo sasa na vijavyo.

Awali mkutano huo wa siku tano ulifunguliwa na Mkurugenzi mkuu wa TAEC Nhini Profesa Lazaro Busagala ambapo unatarajiwa kumalizika kesho .

Mwisho

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: