Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifungua
mkutano wa 53 wa utabiri wa msimu wa vuli kwa nchi 11 za pembe ya
Afrika unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi
akizungumza katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Hayat
Regency jijini Dar es salaam leo.
Meza Kuu
SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) nchini,
kutoa taarifa na tahadhari za mapema za hali ya hewa kwa vile ni muhimu
katika kufikia maendeleo endelevu ya kijamii na uchumi katika nchi zetu
na ukanda wote Wa pembe ya Afrika
Waziri Wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasikiano Mhandisi Izack Kamwelwe
amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam alipofungua mkutano wa 53 wa
utoaji wa utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa mvua za vuli kwa nchi 11
za pembe ya Afrika.
Mhandisi Kamwelwe amesema ni vema utabiri ukatolewa kwa wakati
sababu nchi nyingi za ukanda huo ikiwemo Tanzania zinategemea sana hali
ya hewa.
"Sekta Kama vile kilimo na usalama wa chakula, maji, Nishati, Afya,
Mifugo, uvuvi na shughuli nyinginezo zinazofanyika baharini,
usafirishaji na utalii na nyingine nyingi hutegemea sana hali hewa hivyo
mabadiliko ya hali hewa yanayoambatana na vipindi virefu vya ukame na
mvua yanaendelea kuufanya utabiri kuwa Wa umuhimu sana..
Aidha, Kamwele ameshauri kutumia pia njia za asili za kutabiri hali
ya hewa kuliko kuachana nazo kabisa huku akisisitiza kwamba njia hizo
zinaweza kuboreshwa.
"Hata wakati wa kubadili sheria kutoka kwenye Agency kwenda kwenye
Authority tulipata ushauri kwamba hata kakakuona tunaweza kumtumia
kuandaa utabiri," alisisitiza Waziri Kamwelwe.
Waziri huyo aliwataka washiriki 200 wa mkutano huo watatoka na
maazimio yatakayochangia upatikanaji wa taarifa sahihi zaidi za hali ya
hewa ili kuwasaidia watumiaji wa taarifa hizo kwenye shughuli zao za
maendeleo kwa nchi shiriki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agnes Kijazi amesema wataalam
hao pamoja na kujadiliana na kukubaliana na kufikia muafaka Wa pamoja
juu ya utabiri wa hali ya hewa wa msimu ujao wa mvua za vuli Oktoba hadi
Desemba watatoka na utabiri wa nchi wanachama kwa maendeleo ya nchi
zao.
"Hii ni mikutano inayofanya mara kwa mara kabla ya kuandaa taarifa ya
msimu kwenye nchi zetu huwa tunakutana na kutoa utabiri wa ukanda wetu
huu na mwaka huu kauli mbiu yake ni utoaji wa tahadhari kwa hatua za
haraka katika kukabiliana na athari za hali mbaya ya hewa.
"...Naamini mkutano huu utakuwa na matokeo chanya hivyo basi
watumiaji wa taarifa zetu waendelee kusubiri," alisema Dk. Kijazi huku
akifurahia Tanzania kupewa heshma ya kuandaa mkutano huo muhimu Afrika.
Amesema ingawa kuna changamoto kubwa upungufu wa hali ya hewa,
Tanzania imejenga miuondombinu ya hali ya hewa ikiwemo kujenga rada na
tayari mpaka sasa kina rada mbili na Tatu ziko katika hatua ya manunuzi
ambapo mpango wa TMA ni kuwa na rada saba.
Akizungumzia mvua zinazoendele kunyesha, dk. Kijazi amesema kuwa
zipo nje ya msimu huku akibainisha kwamba ni mabadiliko yanayosababisha
kupungua kwa mkandamizo wa hewa baharini jambo linalosababisha unyevu
kwenye anga.
"Sio mvua kubwa na hazitachukua muda mrefu, hizi zipo hasa ukanda wa
Pwani na mikoa inayozunguka Ziwa Victoria... Wananchi wasihofu," alisema
Dk. Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TMA, Burhani Nyanzi alisema
mkutano huo unalenga kuwasaidia watu wote wanaofanya shughuli zao
wakitegemea hali ya hewa.
Kongamano hilo linahusisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka nchi
mbali mbali zikiwemo, Tanzania, Ethiopia, Sudan, Sudan ya kusini
Burundi, Djibouti, Elitrea, Kenya, Somalia, Uganda nw Rwanda.
Post A Comment: