Waziri
wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu
akizungumza mara baada ya kukutembelea moja ya meza za vipodozi
vilivyokuwepo katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu
alipotembelea moja ya meza za vipodozi lipotemelea meza ya kutengeneza
mawigi katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu
akizungumza na wadau wa urembo mara baada ya kukutembelea meza za
vipodozi vilivyokuwepo katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa urembo wakimsikiliza Waziri
wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu
katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Na Leandra Gabriel
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu
amesema kuwa ongezeko la wagonjwa wa Kansa kutoka taasisi ya Kansa Ocean
road imefikia wagonjwa 7649 mwaka 2018 ukilinganisha na wagonjwa 2416
mwaka 2015.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa chama Cha urembo na
vipodozi nchini (TCA), Waziri Ummy amesema kuwa amesukumwa sana
mapinduzi yanayofanywa katika sekta ya urembo na vipodozi na amesukumwa
zaidi kuhudhuria ufunguzi huo na akiwa mwanamke mwenye dhamana katika
Wizara inayosimamia jinsia pia ameona hilo ni jambo jema la kuungwa
mkono hasa sekta hiyo inahusisha afya pia.
Amesema
kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa ya ini, figo, moyo na
saratani ambapo kwa mwaka 2015 wagonjwa wa kansa walikuwa 2416 hadi
kufikia wagonjwa 7649 kwa mwaka 2018 na sababu mojawapo inayosababisha
ni matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu vikali na amewashauri
watengenezaji wa vipodozi kutengeneza mazingira bora ya biashara kwa
kutengeneza bidhaa zinazokidhi viwango huku akiahidi ushirikiano katika
suala zima la upatikanaji wa masoko.
Waziri
Ummy amewapongeza waanzilishi wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti
wao Shekha Nasser kufanikisha kuanzishwa kwa chama hicho na wao kama
Wizara watahakikisha wanatengeneza mazingira bora ya biashara ili
kuendeleza ujenzi wa viwanda pamoja na kuuza na kufanya biashara nje ya
nchi.
Vilevile
amewashauri Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) pamoja
na baraza la taifa la elimu ya ufundi (NACTE) kuweka sehemu ya mafunzo
katika sekta urembo katika mitaala ya elimu ili hata watu kutoka nje ya
nchi waweze kuja kujifunza masuala ya urembo nchini na kuzidi kuipa
thamani sekta hiyo, pia amewahakikishia wanachama hao kuwa serikali
itaendelea kukuza sekta hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Vilevile
ametoa rai watengenezaji na wauzaji wa vipodozi na urembo kufuata
kanuni na taratibu pamoja na kuwashauri watanzania kukitumia chama hicho
ili kuwe na sauti moja ya kuwasiliana na kufanya maamuzi kwa manufaa
yao na taifa kwa ujumla.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa chama hicho Shekha Nasser
amesema kuwa tasnia hiyo inakua haraka duniani, barani Afrika na nchini
Tanzania na kwa mwaka 2017 pekee ilikuwa na thamani ya dola za
kimarekani bilioni 532 duniani huku ikitegemewa kufikia dola bilioni 863
kwa mwaka 2024 kwa ukuaji wa asilimia 7 kwa mwaka.
Amesema
kuwa kuanzishwa kwa chama hicho kumelenga kufanikisha malengo
mbalimbali yakiwemo kuwaunganisha wadau wote wa sekta ya vipodozi na
urembo pamoja na kukusanya maoni na kuyapeleka kwa serikali yakiwa na
sauti moja na hiyo ni pamoja na kuendeleza viwanda vidogo, vya Kati na
vikubwa na vinachangia sana katika kukuza ajira kwa vijana, kulipa kodi
na mapato kwa serikali.
Shekha
amesema kuwa Tanzania inapata asilimia 3 pekee katika soko la dunia
huku wanufaika wakubwa wakiwa ni nchi za Afrika kusini, Kenya na
Nigeria.
Post A Comment: