FARIDA SAIDY, MOROGORO
Naibu
waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe.Constantine Kanyasu
ameagiza kukamatwa kwa wananchi wote waliovamia na kukata miti bila
kufuata taratibu za kisheria katika msitu wa hifadhi ya kijiji cha
Kumbulu uliopo wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Naibu
waziri ameyasema hayo alipotembelea eneo hilo na kujionea uharibufu
mkubwa uliofanywa na baadhi ya wananchi waliovamia msitu huo licha ya
kufahamu eneo hilo lilitengwa kuwa hifadhi ya serikali ya kijiji tangu
mwaka 2008 akilenga kutafuta ufumbuzi wa mgogoro baina ya serikali ya
kijiji na wananchi.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo Bi. Siriel Nchemba amesema mgogoro
huo umedumu kwa muda mrefu na hatua za ufumbuzi kwa ngazi ya wilaya
zilielekea kushindikana, kutokana na vitisho kutoka kwa viongozi wa juu
serikalini ambapo tayari baadhi ya viongozi wameondolewa katika nafasi
zao.
Post A Comment: