






Na Dixon Busagaga,Moshi
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja mambo 15 aliyofanya Rais John
Magufuli kwa kipindi cha miaka minne alichokaa madarakani na kuwataka
watanzania kumuunga Mkono.
Ndugai
ameyataja mjini Moshi, wakati wa
kongamano la kumpongeza Rais lililoandaliwa na Umoja wa wanawake wa
Chama cha Mapinduzi (UWT).
Hotuba
ya Ndugai ilisomwa kwa niaba yake na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson , katika uwanja wa Majengo na kuhudhuriwa na wanachama wa UWT na
wanawake wa mkoa huo.
Ndugai
alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, imetekelezwa kwa
kiwango kikubwa,na kwamba miongoni mwa mambo ambayo ametekeleza Rais ni
kurejesha nidhamu kwa watumishi.
Alisema
lingine ni kushughulikia tatizo sugu la Rushwa ndani ya serikali,na
ndani ya chama cha mapinduzi hali ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa
rushwa ya uchaguzi katika Chaguzi zijazo.
Akizungumza
mwenyekiti wa UWT Taifa, Gaudensia Kabaka, alisema kongamano hilo
lililenga kumpongeza Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha
miaka minne na kwamba mambo makubwa yamefanyika katika kipindi hicho.
Mwisho
Post A Comment: