Mfamasia
kutoka Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando akitoa mafunzo kuhusu njia
bora ya kujikinga na kudhibiti maambukizi wakati wa kumuhudumia mgonjwa
kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Afisa
kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akijibu hoja kutoka
kwa moja ya washiriki wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya
kujikinga na kudhibiti maambukizi kwa kufuata taratibu za utoaji huduma
kwa mgonjwa (IPC guideline).

Afisa
kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Radenta Bahegwa akielekeza jambo
wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na
kudhibiti maambukizi kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji
huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).

Picha
ya pamoja ikiongozwa na Maafisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa
Huduma Wizara ya Afya na Timu ya Wataalamu wa Afya ngazi ya Mkoa (RHMT)
wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na
kudhibiti maambukizi kwa taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC
guideline).
*****************
Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-KAGERA
Asilimia
56 ya vifo vya watoto wachanga husababishwa na magonjwa yanayotokea
wakati wa utoaji huduma za Afya (Healthcare Associated Infections)
katika nchi zinazoendelea.
Hayo
yamesemwa na Afisa kutoka kitengo cha uhakiki ubora wa huduma kutoka
Wizara Afya Dkt. Radenta Bahegwa kwenye semina ya mafunzo ya njia bora
ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni,
miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa IPC Guidline)
Alisema
taarifa ya tafiti inasema kuwa 75% ya vifo hivyo vilitokea katika nchi
zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo nchi ya Tanzania, huku
ukosefu wa huduma ya maji safi yakutosha katika baadhi ya zahanati
ikionekana ni moja ya changamoto iliyosababisha tatizo hilo la vifo.
“Tafiti
zinaonesha kuwa, 42% ya Vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyo na
wodi za kujifungulia havikuwa na maji na vifaa kwaajili ya kuoshea
mikono, hali inayopelekea kuwa katika hatari yakupata maambukizi kwa
vichanga, mama zao au Watoa huduma”.
Aidha,
alisema kutofuata kanuni na taratibu za utoaji huduma kwa wagonjwa kwa
baadhi ya Watoa huduma ni moja kati ya visababishi vikubwa vya vifo vya
vichanga vingi katika nchi zinazoendelea, jambo linalorudisha nyuma
maendeleo ya Sekta ya Afya katika nchi hizo ikiwemo Tanzania.
Hata
hivyo alisisitiza kuwa ni muhimu kwa Watoa Huduma kufuata misingi na
taratibu za kutoa huduma kwa Wagonjwa (IPC Standard) ikiwemo kunawa
mikono ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi yanayotokea wakati wa
utoaji huduma kwa Wagonjwa ikiwemo vichanga (Healthcare Associated
Infections).
“Usafi
wa mazingira kwa kufuata kanuni za usafi katika maeneo ya kutolea
huduma za Afya, hauishii kusafisha maeneo tu, bali hata kupangilia kila
kitu ili kikae katika eneo linalostahili”. Alisema Dkt. Radenta
Bahegwa.
Aliongeza
kuwa kuweka mazingira safi kutasaidia kupunguza hatari za maambukizi
kwa Mgonjwa au kwa Watoa huduma, pia kunaongeza hamasa ya kufanya kazi
kwa bidi kwa Watoa huduma na kuvutia wagonjwa jambo litalosaidia
kuongeza mapato katika Kituo cha Afya.
Kwa
upande wake Afisa Afya, Mazingira kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali
(JBHN) Bw. Said Chibwana alisema kuwa, Lazima kuwe na choo angalau
kimoja kwa kila watumiaji 20 kwa wagonjwa wa ndani, na watumiaji wote 25
kwa Wagonjwa wa nje.
Alisema
upatikanaji wa huduma za maji safi katika Vituo vya kutolea huduma za
Afya husaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia maambukizi ya ugonjwa, kulinda
Afya za watoa huduma na Wagonjwa wakati wa utoaji wa huduma za Afya
Post A Comment: