Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati
akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo
kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni
2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati
akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo
kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni
2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara
mbalimbali zimeanza ushirikishwaji wa kujadiliana kuhusu utekelezaji wa
Sera ya Kilimo ya Taifa ya Mwaka 2013 na kutoa maoni yao kuhusu
mapendekezo ya kurekebisha Sera hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameyasema hayo wakati
akifungua kikao kazi cha wadau kuhusu marekebisho ya sera ya Kilimo
kinachofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Morena tarehe 13 Juni
2019.
Mhandisi
Mtigumwe amesema kuwa Maboresho hayo yanalenga kuhuisha shughuli za
kilimo ili ziendane na mahitaji halisi ya nchi ikiwa ni pamoja maendeleo
ya viwanda.
Alisema,
timu ya Wataalamu ya Wizara ya Kilimo inaendelea na ukusanyaji wa maoni
kutoka kwa Wadau maeneo mbalimbali ya nchi ikizingatia pia ushiriki wa
makundi mbalimbali ya Kijamii.
Katika
kikao kazi hicho Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa fursa hiyo ya
kushirikishwa katika mchakato wa mapitio ya marekebisho ya Sera ya
Kilimo, ni heshima kubwa kwa wadau hao. “Hivyo, nawasihi wadau wote
mshiriki kikamilifu kutoa maoni yenu kwa uwazi na uhuru ili kuakisi
uaminifu mliopewa na Wizara ya Kilimo. Aidha, maoni yenu ni muhimu
katika maboresho ya Sera ya Kilimo yatakayochochea ukuaji wa sekta ya
kilimo ambayo hutegemeana na sekta nyingine katika ukuaji wa uchumi kwa
lengo la kufikia uchumi wa kati” Alikaririwa Mhandisi Mtigumwe
Kadhalika
alisema pamoja na mambo mengine lakini wadau watapata fursa ya kutambua
jitihada za Serikali zinazoendelea katika kurekebisha Sera ya Kilimo ya
Mwaka 2013 na kutoa maoni yao kwa uwazi na uhuru katika marekebisho ya
Sera yanayopendekezwa.
Aidha,
Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa pamoja na ukweli kwamba, Wizara imeandaa
Rasimu ya Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Kilimo ya Taifa ya Mwaka,
2013 pamoja na uchambuzi unaoainisha mapungufu ya awali (gap analysis).
Hata hivyo, kikao hicho kitatoa mwanga zaidi wa mapungufu yaliyopo na
kuyaainisha kabla ya kuendelea katika hatua zinazofuata.
MWISHO
Post A Comment: