Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole
ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro wa wananchi
wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Hata hivyo Waziri
Kigwangalla ameumaliza mgogoro huo kwa kuagiza wakazi hao wapewe kibali cha
ujenzi na mamlaka hiyo katika eneo lililopendekezwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akisikiliza maoni na hoja za wananchi wa Kata ya Alaitole alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo lao la Esere, wilayani Ngorongoro jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe.William Ole Nasha akizungumza na wakazi wa Kata ya Alaitole iliyo ndani ya Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ilizuiwa kujenga shule ya bweni ya wasichana na mamlaka hiyo zuio ambalo limeondolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii aliyefika katika kata hiyo kutatua mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, viongozi na wananchi wa Kata Alaitole wakitazama eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale lililogunduliwa na wakazi hao katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Taarifa kuhusu fuvu hilo zinaendelea kufanyiwa utafiti na watalaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kupitishwa na katika eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale ambalo bado taarifa zake zinaendelea kufanyiwa utafiti katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro.

Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe.William Ole Nasha na askari wa uhifadhi
wakiangalia eneo itakapojengwa shule ya wasichana ya bweni ya kata ya Alaitole.
Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana kwa furaha na wananchi wa Kata
ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro
wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. PICHA/
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamisi Kigwangalla na wananchi wa Kata ya Alaitole katika Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro. Mhe. Kigwangalla alifika kutatua mgogoro uliohusisha wananchi wa
Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya
NgorongoroWMU
– Ngorongoro, ARUSHA.
11/6/2019.
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro uwaruhusu wananchi wa Kata ya Alaitole wajenge shule ya wasichana ya bweni katika eneo la
Esere lililo ndani ya Mamlaka hiyo ili waweze kupata elimu kufuatia wananchi
hao kuzuiwa kwa muda mrefu kutekeleza mradi huo.
Aidha, ameutaka
uongozi wa Mamlaka hiyo utoe kibali cha kuwawezesha wananchi kata hiyo kuanza ujenzi
haraka iwezekanavyo ili fedha zilizotolewa na Serikali shilingi milioni 298 zianze
kutumika.
Dkt. Kigwangalla
ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa
Kata Alaitole wilayani Ngorongoro kwenye mkutano wa hadhara uliowashirikisha
viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, viongozi serikali wa kata hiyo, viongozi wa mila wa
kabila la Masai na madiwani na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha.
Amesema Serikali
inaunga mkono juhudi zote za wananchi za kujiletea maendeleo akifafanua kwamba
hatua ya wananchi hao kuamua kujenga shule ya Sekondari ya Bweni ni jambo la
linalopaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo.
“Mnacho kitaka kiko
wazi, mnataka maendeleo ya watoto wenu, katika hili mmesema kila baba anatoa
elfu hamsini na wanawake wanatoa elfu ishirini, hili ni jambo kubwa achilia mbali nguvu kazi mnayojitolea na tayari
serikali imeshaleta milioni 298, haiingii akilini eneo linalochangia kuleta na
kuingiza mapato mengi Serikalini kiasi cha bilioni 126 likose shule”
Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangalla
ameeleza kuwa ujenzi shule hiyo utawaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali
mrefu akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye
mipango yao ya utekelezaji miradi ya maendeleo.
Amesema jamii hiyo
pamoja na mazingira wanayoishi kuwa ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wanahitaji
elimu. Aidha, amesema pia ni muhimu katika sekta ya utalii kupitia utamaduni
wao akiongeza kuwa kazi ya Wizara ni kuona mafanikio ya sekta ya utalii
yanakuwa kwa kuongeza mapato na sio migogoro.
Dkt. Kigwangalla amesema
Hifadhi ya Ngorongoro ni hifadhi mseto inayoruhusu binadamu na wanyama kuwepo katika
eneo moja na kwamba hiyo ipo kwa mujibu wa sheria akiitaka Mamlaka hiyo kuyatazama
vizuri majukumu yake ya kuendeleza Utalii, Kulinda rasilimali zililizopo kwa
maana ya kuhifadhi na kuhudumia jamii iliyo ndani ya hifadhi hiyo.
Katika hatua nyingine
ameutaka uongozi wa Mamlaka hiyo uendelee kufanya mazungumzo na wananchi hao
badala ya kujielekeza katika matumizi ya nguvu ili kupata uelewa wa pamoja
akitolea mfano wa eneo la Loliondo ambalo hivi sasa lina utulivu.
“ Viongozi wa Mamlaka
mnalo jukumu la kuwasikiliza wananchi na kuamua kwa pamoja, eneo la Ngorongoro
ni Urithi wa dunia na litaendelea kuwa hivyo kwa kuheshimu na maslahi ya Taifa
na maslahi ya walio walio wengi” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
Kuhusu mahusiano baina
ya wananchi na wahifdhi Dkt. Kigwangalla amesema kuwa kupitia mkutano wake na
wananchi amebaini kuwepo kwa tatizo la mawasiliano na mahusiano baina ya
wananchi wa eneo hilo na watumishi wa
Serikali walio chini ya Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro akibainisha kwamba tayari serikali imeliona jambo hilo na
inaendelea kulifanyia kazi.
Naye Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe.
William Ole Nasha akizungumza wakati wa mkutano huo amempongeza na kumshukuru Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa kazi kubwa anayoifanya ya
kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za Taifa katika maeneo mbalimbali nchini.
Amemwomba aeendelee
kutembelea maeneo mengine ya jimbo hilo kwa lengo la kusikiliza kero za
wananchi wa kata za wilaya hiyo kwa lengo la kudumisha mahusiano mema.
Mhe. Ole Nasha
ameeleza kuwa hatua ya Wizara kutafutia ufumbuzi mgogoro huo wa ujenzi wa shule
ya wasichana ya bweni, vile vile uamuzi wa serikali kutoa eneo na fedha kiasi
cha shilingi milioni 298 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo katika eneo
lililokubaliwa ni ishara tosha kwamba Serikali inawalinda na kuwajali wananchi
wake.
Amesema wananchi wa
jimbo la Ngorongoro pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wako ni wasikivu
na wako tayari muda wote kushirikiana na Serikali ikiwemo ulinzi wa rasilimali
zilizopo na kuendeleza uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro.
Kwa upande wao wananchi
wa Kata ya Alaitole wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru Dkt.
Kigwangalla kwa kuamua kuwafuata na kuzungumza nao katika makazi yao wakimpongeza
kwa juhudi zake za kutatua changamoto mbalimbali kwa maslahi ya wananchi na
uhifadhi.
Aidha, wamemwomba kuendelea
kuisimamia sekta ya uhifadhi nchi wakitoa wito wa kudumisha mahusiano mema
baina ya wananchi na wahifadhi.
MWISHO
Post A Comment: