Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati
akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao makuu sambamba na
wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za
COASCO makao makuu Jijini Dodoma leo tarehe 3 Juni 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati
akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao makuu sambamba na
wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za
COASCO makao makuu Jijini Dodoma leo tarehe 3 Juni 2019.
Sehemu ya watumishi wa COASCO wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati
akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao makuu sambamba na
wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za
COASCO makao makuu Jijini Dodoma leo tarehe 3 Juni 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Uongozi
wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)
limetakiwa kukagua vyama vote vya Ushirika na kuwasilisha taarifa ya
ukaguzi huo ofisi ya Waziri wa Kilimo kwa ajili ya hatua stahiki.
Mhe
Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa Kilimo ametoa agizo hilo leo tarehe 3
Juni 2019 wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao
makuu sambamba na wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika
katika ofisi za COASCO makao makuu Jijini Dodoma.
Alisema
kuwa lengo kuu la COASCO ni kuhakikisha kuwa vyama vya ushirika
vinakidhi matakwa ya kisheria na misingi ya kuanzishwa kwake ili
wanaushirika na vyombo vyao vinakuwa salama kulingana na makubaliano,
katiba na sheria zilizopo vile vile kusimamia sheria za ushirika na
sheria za biashara wanazofanya ikiwa ni pamoja na sheria na sera za nchi
na utawala bora.
“Nakuagiza
Kaimu Mtendaji Mkuu kuhakikisha kuwa unakagua vyama vyote vya ushirika,
mimi nisingependa nikikuomba ripoti ya ukaguzi uniambie eti kuna vyama
vingine hujakagua na taarifa ya ukaguzi iwasilishwe katika ofisi yangu”
Alisisitiza Mhe Hasunga
Aliongeza
kuwa huduma za ukaguzi zinazotolewa na Shirika zinasaidia kuimarisha
utawala bora katika vyama vya ushirika, kuwajengea imani wanachama wa
vyama vya ushirika juu ya shughuli zinazofanywa na vyama vyao na hivyo
kuongeza uzalishaji na kuboresha huduma zinazotolewa na vyama vya
Ushirika.
Mhe
Hasunga pia alimuagiza kaimu Mtendaji mkuu huyo kuhakikisha kuwa
anapeleka mapendekezo ya viongozi waliopo katika vyeo vyao ili kuweza
kuthibitishwa kwa wale wanaostahili.
Kwa
kutambua mchango wa ushirika katika mageuzi ya kiuchumi hasa kwa wakati
huu ambao serikali ya awamu ya tano inakusudia kuingia katika uchumi wa
kati (kupitia agenda ya Tanzania ya Viwanda), Hivyo ili kufanikisha
agenda hiyo wametakiwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato.
Aliongeza
kuwa Vyama vya ushirika vina nafasi kubwa kuinua uchumi ikiwa tu
usimamizi wa sheria na kanuni utaimarishwa kama inavyojidhihirisha
katika serikali ya awamu ya tano.
Alibainisha
pia kuwa, udhaifu katika usimamizi wa mifumo ya ufatiliaji ni moja ya
changamoto zilizosababisha vyama vingi vya ushirika kutumbukia katika
matatizo na kupelekea vyama vingi kufilisika.
Shirika
la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) ni Shirika la
Umma lililoanzishwa kwa Sheria Na. 15 ya mwaka 1982 kwa lengo la kutoa
huduma za ukaguzi na Usimamizi kwa Vyama vya Ushirika Tanzania.
Sheria
hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2005 ili kupanua wigo wa huduma za
Shirika za Ukaguzi na Ushauri kutolewa kwa vyama vya ushirika pamoja na
taasisi za Umma, makampuni binafsi, mabenki na wateja wengine.
MWISHO
Post A Comment: