Mkuu
wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kaundasuti nyeusi) akiongozana na
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura pamoja na kamati ya
ulinzi na Usalama ya Mkoa na wataalamu wengine wakati wa ukaguzi wa
ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kaundasuti nyeusi) akiongozana na wataalamu kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kaundasuti nyeusi) akiongozana na wataalamu kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kalambo.
Jengo la Maabara la Hospitali ya Wilaya ya Kalambo likiwa katika hatua ya Kenzi tayari kwaajili ya kuezekwa. |
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangapo amemuagiza mkuu wa Wilaya ya
Kalambo pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya kuwasaka na
kuwatia nguvuni wananchi wanaosadikiwa kuhujumu miundombinu ya maji
katika Kijiji cha Kisongamile ambacho kipo jirani na ujenzi unaoendelea
wa hospitali ya wilaya ya kalambo hali inayopelekea kurudisha nyuma kasi
ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema
kuwa hospitali hiyo ni ya kwao na kwamba wao ndio wa kwanza kufaidika
na ujenzi wa hospitali hiyo pindi itakapokamilika, hivyo amemtaka mkuu
huyo wa wilaya kuhakikisha analimaliza tatizo hilo ndani ya muda mfupi
ili kuendana na ratiba ya umaliziaji wa ujenzi wa hospitali hiyo.
“Nimeona
hii changamoto ya maji pamoja na kwamba wanachimba kisima, lakini kile
Kijiji pale ambacho kinakwamisha kinahujumu miundombinu ya maji Mhe. DC
pamoja na kamati ya usalama muende pale, pamoja na mwenyekiti wa
halmashauri, mkazungumze na kile Kijiji, lakini pia kama kuna watu ambao
wanadhaniwa wanahujumu kwa makusudi miundombinu, haiwezekani Kijiji
kizima kikawa kinahujumu miundombinu, mchukue hatu ya kuwakamata hao
wote wanaohujumu miundombinu ya maji,” Alisisitiza.
Aidha,
alieleza kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa hoapitali hiyo ambapo mpaka
tarehe 8.6.2019 bado wapo katika hatua ya kuweka kenchi na huku
hawajaanza kuweka plasta wala kununua vifaa vingine kama milango,
madirisha, vigae na mabomba na hivyo kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kalambo kuhakikisha wananunua vifaa hivyo mapema ili
inapofikia hatua ya kuvipachika vifaa hivyo kusiwepo na usumbufu.
Halikadhalika
amewataka mafundi wanaosimamia majengo ya hospitali hiyo kuhakikisha
wanapiga plasta majengo yote na kutahadharisha kuwa fundi yeyote
atakayepitisha muda wake bila ya kumaliza jengo itambidi fundi huyo
kuilipa serikali na kusisitiza kuwa serikali haitaongeza hata siku moja
katika kuhakikisha majengo hayo yanakamilika.
Ameyasema
hayo alipotembelea eneo la ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kalambo
inayotakiwa kukamilika ifikapo tarehe 30.6.2019 akiongozana na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na wataalamu kutoka katika ofisi yake.
Awali
akielezea changamoto ya kusuasua kwa upatikanaji wa maji katika eneo
hilo la ujenzi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Msongela
Palela alisema kuwa miongoni mwa changamoto kubwa ni uhujumu wa
miundombinu ya maji inayoelekea kwenye ujenzi wa hospitali hiyo
unaofanywa na wananchi wa Kijiji cha Kisongamile huku sababu kubwa ya
uhujumu huo ni Kijiji hicho kukosa umeme.
“Changamoto
nyingine ni ya hawa wenzetu wa Kijiji cha Kisongamile, ambao wao
wanasema kwamba walipaswa kuwa wamepata umeme ambao mpaka sasa hawana
umeme, kwahiyo kwasababu hiyo hii miundombinu ya maji wataendelea
kuihujumu mpaka pale watakapokuwa wamepatiwa umeme, tunaendelea
kuwaelimisha na kukaa nao kuwashauri kwamba wanachofanya ni hujuma kwa
serikali yao lakini nimshukuru mkuu wa Wilaya ameshachukua hatua za
awali kwamba wanaohujumu watambuliwe na kuchukua hatua,” Alisema
Pia,
alisema kuwaendapo wananchi hao hawatadhibitiwa huenda wakati
zitakapoanza opereshi za hospitali chnagamoto hiyo ikajitokeza hivyo ili
kuhakikisha kwamba tahadhari inachukuliwa na kuwa hospitali inakuwa na
maji wakati wote ndio maana tunakwenda kwenye wazo mbadala la kuchimba
kisima.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa Wilaya ya Kalambo Dkt. Allen Kalekwa wakti
akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa hospitali hiyo alisema kuwa baadhi ya
vifaa kwaajili ya umeme, bati na mbao za kenchi zimeshanunuliwa na
vingine vipo njiani na kuwa hadi kufukia hatua hiyo tayari halmashauri
imeshatumia shilingi milioni 940 na kubakiwa na shilingi milioni 560
ambazo ni kwaajili ya kununua vifaa kama, marumaru, aluminian, gypsum na
fedha ya mafundi na kisha kueleza changamoto ya maji.
“changamoto
kubwa tuliyonayo kwa sasa ni tatizo la maji, tulishafunga mfumo wa maji
mpaka hapa yalikuwa yanakuja lakini bahati mbaya kuna baadhi ya sehemu
wanakata mabomba ya maji, lakini hatua za awali mpaka sasa hivi
tumeshanunua madumu matatu ya lita 15,000 ya kuhifadhia maji na wenzetu
wa ujenzi wa barabra wanatusaidia kutujazia maji lakini pia tunatarajia
kuchimba kisima kwaajili ya utatuzi wa muda mrefu,” Alisema.
Post A Comment: