picha ikionyesha kiongozi wa Mbio za mwenge  wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee mkongea Ally akikata utepe ishara ya kuzindua mradi wa maji wa layout srwsita uliopo katika halmashauri ya Arusha Dc
 Picha ikionyesha kiongozi wa mwenge wa uhuru  kiongozi wa Mbio za mwenge  wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee mkongea Ally akifungua shule ya sekondari ya odonyowas
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikabithiwa mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe tayari kabisa kwa kumbizwa katika wilaya ya Arumeru ambapo katika wilaya hii ina halmashauri mbili ambapo jumla ya miradi nane imezinduliwa Katika halmashauri ya Arusha na katika halmashauri ya Meru jumla ya miradi itakaguliwa na baadhi kuzinduliwa

Na Woinde Shizza, Arusha 
Wananchi wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuendeleza kumpinga adui ujinga pamoja na kutunza vyanzo vya maji kwani maji nirasilimali muhimu ambayo inaletea nchi yetu maendeleo. 


Serikali  wameingia mikakati ya kuhakikisha  wananchi wanapata maji safi na salama kwa ajili ya wananchi wao ,Aidha pia serikali imetenga kiasi cha shilingi trilioni 9.2kuhakikisha wananchi wao wanapata maji safi na salama 

Hayo yamebainishwa na kiongozi wa Mbio za mwenge  wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee mkongea Ally wakati akizindua miradi ,kuweka jiwe la msingi pamoja na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo .

Alisema   Maji ni rasilimali nzuri ambayo inachingia kuleta maendeleo ya nchi yetu hivyo wananchi wanatakiwa kutunza mazingira hususa ni vyanzo hivi vya Maji. 

"nakatika swala hili la kutunza vyanzo vya maji napenda kuwasihi wananchi wenzangu kuacha kuchunga mifugo yetu katika vyanzo vya maji pamoja na nakuacha kufanya shughuli za kibinadamu  katika vyanzo vya maji "Mzee mkongea 

Aidha pia alisema kuwa Maji ni haki ya kila mtu hivyo ni wajibu wetu na kila Mwananchi  kutunza vyanzo hivi vya maji 

 Alisema kuwa hivi karibuni tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za vijiji pamoja na mitaa hivyo aliwataka wananchi hususa ni vijana pamoja na wamama kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ambazo zinagombaniwa 

Pia aliwataka wananchi kujitokeza kusikiliza sera za wagombea hao na kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi ambaye ataweza kuiongoza vyema na kuwaletea wananchi maendeleo

"wananchi wenzangu jitokezeni kusikiliza sera za hawa viongozi wanaogombea ili muweze kufanya uchaguzi sahihi katika chaguzi za serikali zijaazo na msichague bora kiongozi bali chagueni kiongozi bora"mzee mkongea 


Alimalizia kwakuwataka  wananchi kulipa kodi kwani Kodi ndio msingi wakuleta maendeleo ya taifa letu, kwani kwakufanya hivyo ndiko kunatusaidia kuleta maendeleo katika halmashauri zetu na hata vijiji vyetu  
 
Katika mbio hizi za mwenge katika halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc  imezindua miradi mbalimbali ikiwemo kuzindua na kufungua shule Ya sekondari ya Odonyowas, mradi wa maji wa layout Srwsita,mradi wa Nyuki pamoja na hospital ya mama na mtoto ya orturmenti.
Share To:

Post A Comment: