Afisa Sheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Mkoani Tanga Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo wakati wa warsha ya klabu za ardhi kwa shule za sekondari na Kilulu na Magila iliyohusisha wanafunzi nane kila shule na walimu wawili na kufiia jumla yao washiriki ishirini
Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo akizungumza wakati wa warsha hiyo ambapo alisema uanzishwaji wa klabu hizo utasaidia kupunguza changamoto zilizopo kwenye jamii kutokana na baadhi yao kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala la ardhi
Sehemu ya walimu na wanafunzi wakichukua dondoo wakati wa warsha hiyo

Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa rsha hiyo
WANANCHI wa Mkoa wa Tanga ambao wamekuwa na tabia za kutoku huisha maeneo ya ardhi wanayomiliki kihalali baada ya kupita miaka 35 wamepewa tahadhari kwamba wanaweza kujikuta wakipoteza sifa za kuendelea kuwa wamiliki kwa mujibu wa sheria.

Kwani hatua hiyo inatokana na kwamba asilimia kubwa baada ya kupata umiliki wa ardhi wanashindwa kutambua kwamba kila baada ya miaka hiyo kupitia wanapaswa kwenda kuyahuisha kisheria badala yake wamekuwa wakiendelea kumiliki.

Hayo yalisemwa na Afisa Sheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Mkoani Tanga Mwanaidi Kombo wakati wa warsha ya klabu za ardhi kwa shule za sekondari na Kilulu na Magila iliyohusisha wanafunzi nane kila shule na walimu wawili na kufiia jumla yao washiriki ishirini.

Klabu hizo zimeanzishwa kwenye shule hizo kupitia mradi wao wa kuwezesha upatikanaji wa haki za wanawake katika kumiliki, kupata, kutumia na kufanya maamuzi juu ya ardhi na mali jambo ambalo litawawezesha kuwasaidia kuondoa vikwazo kwenye jamii.

Alisema kutokana na uzoefu uliopo unaonyesha kwamba watu wengi hawahuishi umiliki wa wa ardhi baada ya kupitia miaka thelathini na tano kwa sababu wanajiona ni wamiliki tu .

 “Uhalisia ardhi inapofikisha miaka 35 baada ya hapo unatakiwa kuihusisha tena kwani kuna hatari unaweza kunyang’anywa lakini pia uangalie miliki yako ni kubwa au ni ndogo kwani leo serikali inaweza kutangaza watu waliofikisha miaka 35 bila kuhuisha maeneo yao yanachukuliwa na kuuzwa”Alisema Afisa Sheria huyo.

“Asilimia kubwa ya watu wa Tanga wamekuwa hawahuishi maeneo yao baada kupitia miaka inayotakiwa kufanya hivyo hii ni changamoto ikipita miaka 35 bila kuhuisha unakuwa unakosa haki kisheria kumiliki eneo husika”Alisema.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kwamba lazima watazame  hati miliki yao ni aina gani ni kubwa au ni ndogo kama imefikia ukomo au bado lakini kama imefika ukomo waende wakaihuisha kwani iwapo serikali ikisema watu ambao wameshindwa kuihuisha maeneo yao wanachukua ni kweli wanachukua na ni haki yao kisheria.

Awali akizungumza Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo uanzishwaji wa klabu hizo utasaidia kupunguza changamoto zilizopo kwenye jamii kutokana na baadhi yao kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala la ardhi

“Tumeona tutilie mkazo masuala ya elimu mtu anapojua ni rahisi kuweza kukipata na sehemu nyingi walipokuwa wakifanya midahalo imewapa uelewa jamii kuhusu umuhimu wa kupata haki zao”Alisema

Aidha alisema wanawapatia elimu ili waweze kuisambaza kwa wenzao na kuweza kuiendelezaa kwenye klabu zao za mashuleni zinazohusiana na ardhi jambo ambalo litawasaidia kuipa uelewa jamii kuhusiana na changamoto za ardhi zinapojitokweza kwenye maeneo yao.

Hata hivyo alisema wakiwapa elimu hao wakiwa na umri mdogo watakuwa waelewa na kuweza kujitetea na kuweza kutoa elimu kwenye jamii ikiwemo kuwa mabalozi wazuri kuilemisha jamii na kuwa mabalozi wa kutangaza Tawla.

Akieleza sababu za kuendesha mradi huo wilayani humo, Wakili Latifa alisema kwamba Muheza ikiwa ni wilaya yenye wawekezaji wengi na makabila ikiwemo wabondei ambao wanaamini sana mfumo dume.

Alisema kwamba mfumo huo umekuwa hautoi haki sawa kwa mwanamke kwenye kumiliki ardhi ya urithi jambo ambalo limepelekea asilimia kubwa ya wao kuwakosesha haki kuhusiana na haki zao wao hivyo wanachofanya ni kutetea sheria kueielekeza sheria inayosema na sio kufanya watu wagombane.

“Katiba inatambua haki ya binadamu wote ni sawa…kuwafundisha vijana waweze kuwa na uwelewa na kujitambua kuhusiana na masuala ya ardhi kuwawezesha wao kuweza kuwaelekeza vijana wenzao lakini pia kwenda kutoa elimu kwenye jamii kuweza kutatua migogoro iliyopo kwenye jamii”Alisema.
Mwisho.
Share To:

Post A Comment: