Na  Ferdinand Shayo,Arusha.
Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kutengeneza mifuko mbadala ili kuinua vipato vyao na kupunguza tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi  hususan waliohitimu elimu  katika vyuo mbali mbali.
Akizungumza katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya utengenezaji wa mifuko hivyo pamoja na mafunzo ,Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Okoa New Generation Neema Robert amesema kuwa vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo ili kuongeza idadi ya wazalishaji wa vifungashio hivyo na kupelekea bei kuwa rafiki kwa wananchi kutokana na uzalishaji kuongezeka.
Kwa upande wao Vijana waliopatiwa mafunzo ya kutengeneza mifuko  iliyotolewa kwa njia ya vitendo zaidi  Rosemary Shedrack amesema kuwa kwa sasa wameanza kutengeneza mifuko  na kuisambaza katika masokombalimbali pamoja na kujipatia fedha zinazowasaidia kujikimu na kujiendeleza kimaisha.
Mary Daudi  ni moja kati ya vijana wanaotumia fursa hiyo amewataka vijana wengine kuiga mfano na kutumia  fursa hiyo kubadilisha maisha yao kwani vifungashio hivyo vinahitajika kwa wingi nchini baada ya serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki.
Share To:

Post A Comment: