Mwenyekiti wa Taasisi ya "The Desk & Chair Foundation", Sibtain Meghji (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko (kushoto) kifaa cha kusambaza mawasiliano ya mtandao wa Intaneti (Router) pamoja na nyaya za umeme (Cable) ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za chama hicho katika kutimiza vyema majukumu yake ya kihabari katika jamii.
BMG Habari
Taasisi ya “The
Desk & Chair Foundaton” ya jijini Mwanza imeunga mkono juhudi za Klabu ya
Waandishi wa Habari ya Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club-MPC) kwa kukabidhi
miundombinu ya Intaneti.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sibtain Meghjee amemkabidhi
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko vifaa hivyo na kuahidi kuendelea kushirikiana
bega kwa bega na klabu hiyo katika kuchochea maendeleo ya Mkoa Mwanza.
Baada ya
kupokea vifaa hivyo, Soko amesema uwepo wa miundombinu ya Intaneti ya uhakika kwa
waandishi wa habari ni nyezo muhimu katika kutekeleza majukumu yao huku akiishukuru
taasisi ya “The Desk & Chair Foundation” kwa mchango wake katika kuimarisha
shughuli za waandishi wa habari.
Katika hatua
nyingine, Edwin Soko ameongeza kuwa MPC itaendelea kufanya kazi na taasisi ya
The Desk & chair pamoja na wadau mbalimbali wa Mkoa Mwanza pamoja na Serikali
ya awamu ya tano na kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Mwanza.
“Uwezo wa
miundombinu utasaidia waandishi wa habari kutuma habari zao na kupokea taarifa
muhimu na pia kuhudhuria mikutano kwa njia ya mtandao” amesisitiza Soko.
Kifaa hicho (Router) kutoka kampuni ya mawasiliano Tanzania (TTCL) kina uwezo wa kuunganisha kompyuta 30 kwa wakati mmoja hivyo kitasaidia wanachama wa MPC kupata huduma ya intaneti kwa uhakika huku pia wasio wanachama wakichangia gharama kidogo za uendeshaji.
Post A Comment: