Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe
10 Juni 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti
Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali
imearifu kuwa inafanya utafiti na tathmini ya kina ya maji kujaa kwenye
mashamba ya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma
leo tarehe 10 Juni 2019 wakati akijibu swali la Mhe Yahaya Omary Massare
wa Jimbo la Manyoni Magharibi aliyetaka kufahamu serikali ina mpango
gani kuwasaidia wananchi kwa kuwajengea mifereji ya kuongoza maji
yasiingie mashambani.
Mbunge
huyo alisema kuwa Eneo la Mbuga linalozunguka Mji wa Itigi pamoja na
kufaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama Mahindi, Alizeti, Choroko na
Dengu lakini eneo hili linajaa maji na kufanya kilimo kuwa kigumu.
Mhe
Mgumba aliongeza kuwa Utafiti na tathmini hiyo itakapokamilika itakuja
na mikakati na mapendekezo stahiki yatakayosaidia kutatua changamoto ya
kujaa maji mashambani na kuwasaidia wakulima wa eneo la mbuga linalozunguka mji wa Itigi ili kuongeza uzalishaji na tija.
Aliongeza kuwa eneo
la mbuga linalozunguka mji wa Itigi limekuwa likijaa maji pale mvua
zinapokuwa juu ya wastani ambapo historia inaonesha kuwa bonde hili
lilijaa maji kipindi cha mwaka 1997/1998 wakati wa mvua za E-lnino na katika msimu wa 2015/2016 baada ya miaka tisa tangu wakati wa mvua za E-lnino mwaka 1997/98.
Aidha, alisema
kuwa Serikali imelichukua suala la Mheshimiwa Mbunge na itatuma
wataalam wa Kilimo na Tume ya Umwagiliaji kwa ajili ya kwenda kufanya
utafiti na tathmini ya kina ya maji kujaa kwenye mashamba ya wakulima.
Utafiti
na tathmini hiyo itakapokamilika itakuja na mikakati na mapendekezo
stahiki yatakayosaidia kutatua changamoto ya kujaa maji mashambani na
kuwasaidia wakulima wa eneo la mbuga linalozunguka mji wa Itigi ili kuongeza uzalishaji na tija.
MWISHO
Post A Comment: