Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa afisa wa TBA Haruna Kalunga (kulia) wakati alipotembelea ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kalambo.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura
amemkaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo katika ofisi yake
mpya anayotarajia kuhamia mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2019 huku ikiwa
zimebaki asilimia 10 kumalizika kwa jengo hilo tofauti na ofisi ya mpya ya
Mkurugenzi ambayo bado ipo katika hatua za awali za ujenzi.
Mh. Binyura aliwashukuru wakandarasi Suma JKT pamoja na
mshauri wake wakala wa majengo Nchini (TBA) kwa kuweza kuifikisha ofisi hiyo
katika hatua za mwisho kuongeza kuwa pamoja na yeye kuhamia pia anaweza
kushirikiana na mkurugenzi kukaa pamoja ikiwemo kumuazima mabanda yanayozunguka
ofisi hiyo ili aweze kuyatumia wakati wakisubiri kukamilisha ofisi yao.
“Ni kweli jengo hili ni kubwa sana na ofisi hii itatosha
kwa ofisi yangu pia na Mkurugenzi ataingia na pia kuna mabanda mengi tu yapo
hatutayabomoa mapema ili waweze kuingia lakini vile vifaa ambavyo ni vya
kutumia mifumo wataingia kwenye jengo langu, kwahiyo nawakaribisha sana na
wajenzi wajitahidi ili tarehe 30 niweze kuingia kwenye jengo hili,” alisema.
Kauli hiyo imekuja baada ya mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.
Joachim Wangabo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhama katika madarasa
ya shule ya Sekondari ya wasichana Matai ambayo wanayatumia kama ofisi zao.
Mh. Wangabo alisema,” Mh. DC nimesema hawa halmashauri
ofisi zao zitahamia kwako kwa muda utakapokuwa umehamia pale na pale uwape muda
wa kukaa ili uwasukume watoke pale, kama hawatasimamia huu ujenzi hapa wake kule
kwenye vibanda vya kuku kule,wakae kweny vibanda vya mabati ili waone uchungu
wa kusimamia hapa mahali.
Mh. Wangabo aliyasema hayo alipotembelea ujenzi wa ofisi
ya mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Ofiri ya Mkurungenzi wa halmashauri pamoja na
ujenzi wa bwalo na mabweni katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Matai.
Katika hatua nyingine Mh. Wangabo amemuagiza Mkurugenzi
wa halmashauri ya Kalambo kuhakikisha hadi kufikia mwezi Julai mwaka 2019 shule
hiyo iwe imesajiliwa na kuanza kupokea wanafunzi kutoka katika maeneo
mbalimbali ya nchi.
Tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo mwaka 2012
Mkurugenzi amekuwa akitumia madarasa ya shule ya sekondari ya wasichana ya
Matai kama ofisi za halmashauri.
Post A Comment: