Mratibu wa Jinsia na Afya Halmashauri ya Ilala,Rehema Mzungu akizungumza kata ya Buguruni,wakati wa Kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana mafunzo endelevu ambayo yameandaliwa na Manispaa ya Ilala kwa ushirikiano wa Jhpiego Mradi waTCI  tupange pamoja. 

Mwandishi wa habari Kassim Magehe akitoa elimu ya afya ya Uzazi Kwa vijana kata ya Buguruni Walayani Ilala,mafunzo yalioandaliwa na Halmashauri ya Ilala kwa ushirikiano wa Jhpiego mradi wa TCI tupange Pamoja(Picha na Heri Shaaban)

Mkurugenzi wa halmashauri ya Ilala,Jumanne Shauri akizungumza na Watendaji wa Manispaa hiyo Idara ya Afya Ofisi ya Mganga Mkuu Katika Mafunzo ya afya kwa vijana kata ya Buguruni Dar es Salaam

NA HERI SHAABAN

MANISPAA ya Ilala yatoa elimu   ya afya ya uzazi kwa vijana wa Manispaa hiyo ikiwataka vijana waache kujamiana  katika umri mdogo   ili wasipate mimba kabla ya wakati.

Hayo yalisemwa na Mratibu wa Jinsia na Afya Halmashauri ya Ilala Rehema Mzungu Kata ya Buguruni leo, wakati wa ufunguzi  kutoa elimu ya afya ya  uzazi  kwa vijana katika mafunzo  yalioandaliwa na manispaa hiyo kwa ushirikiano wa Jhpiego Mradi wa TCI  Tupange Pamoja  .

Rehema alisema vijana wengi wanafanya ngono katika umri mdogo  wanapata mimba kabla wakati mkakati huo endelevu, wa halmashauri elimu hiyo itasaidia kuepuka mimba zisizo tarajia.


" Halmashauri ya Ilala kwa ushirikiano wa Jhpiego   TCI tupange pamoja tunatoa elimu bure kwa muda wa siku mbili kuelimisha jamii wajiepushe na vifo vya afya ya uzazi ndani ya halmashauri ya Ilala " alisema Rehema.

Alisema elimu hiyo ya afya ya uzazi inatolewa katika vituo vyote vya afya vilivyopo Manispaa hiyo  wananchi wanashauliwa kufika  kupata huduma inatolewa bure.


Aidha alisema elimu ya afya ya uzazi inamsaidia Mama mtoto kujenga afya vizuri  ili aweze pia kujishughulisha kiuchumi na kujenga Taifa.

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum  halmashauri hiyo Helen Ryatula alielezea Madangulo ya Buguruni yanavyochangia vijana chini ya umri mdogo wanavyofanya ngono zembe na kusababisha wengine kupata mimba zisizo tarajiwa.

Ryatula aliwataka Vijana waache kujamiana  kwani ni nguvu kazi ya Taifa wafuate afya ya uzazi kwa Maendeleo .

Naye Mratibu wa Huduma za  Afya ya Jamii Manispaa hiyo Sophia Ntomola, amewataka wazazi kuweka mikakati mbali mbali juu ya malezi ya vijana waache ngono zembe katika umri mdogo ili wapunguze vifo vya Wamama Wajawazito .
Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: