NA HERI SHAABAN
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM wamekabidhi photokopy mashine kwa mikoa 27 Tanzania Bara.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa Dar es Salaam leo kwa mikoa mitatu Tanga,Dar es Salaam na Pwani.
Akikabidhi vifaa hivyo Dar es Salaam leo Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo,Erasto Sima alisema photocopy hizo zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalum Najma Murtaza .
"Mpaka sasa ametoa vifaa vya ofisi katika mikoa
27na Wilaya 12 za Zanzibar vitu vyote vina thamani ya jumla ya shilingi milioni 44 "alisema Erasto.
Erasto alisema bado mikoa Arusha,Mbeya,Njombe,Kilimanjaro na Iringa ilikuwa sehemu ya ahadi yake mbunge huyo wa viti maalum ametekeleza kwa asilimia 95.
Akielezea sehemu zingine aliposaidia photopy hizo kuwa ni Idara ya Siasa Oganaizesheni Wazazi Taifa Dar es Salaam CPU,Ofisi kuu Zanzibar mkoa wa mara wamepata mizinga kumi kwa ajili ya ufugaji nyuki badala ya kompyuta.
Alisema Jumuiya hiyo ya Wazazi ilianzishwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 mwaka 2016 mbunge Najma Murtaza ndio alitoa ahadi hiyo ambayo ametekeleza.
Kwa upande wake Katibu wa Wazazi Tanga Shaban Mdoe akizungumza kwa niaba ya wezake alisema kwa sasa watafanya kazi za chama vizuri.
Mdoe alipongeza kupokea msaada huo ambapo pia alisema kwa sasa siri za chama zitakuwa azitoki nje na kila taarifa za jumuiya zitaandaliwa kwa wakati.
Mwisho
Post A Comment: