Baadhi ya Viongozi wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa wamebeba mabango katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya Madaktari wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa katika matembezi ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Daktari bingwa Upasuaji Mifupa na Majeruhi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina,akizungumza na baadhi ya akina mama wenye watoto wenye ulemavu wa mguu Kifundo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe ,akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe,akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Bw.Emmanuel Kowero katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe,akitoa maelezo kwa Mratibu Miguu Kifundo kanda ya Kaskazini Bw.Goodluck Pallanayo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, akikata utepe mara baada ya kuzindua Cliniki ya Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma

Daktari bingwa Upasuaji Mifupa na Majeruhi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina akiagana na Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, baada ya kuzindua Cliniki ya Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma

Daktari Bingwa Upasuaji Mifupa Hospitali ya Bugando akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

...................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa Mkoa, Dodoma Dkt.James Kiologwe amewaomba wazazi /walezi pamoja na wananchi kutowafungia ndani watoto wenye matatizo ya mguu kifundo.

Watanzania wameungana na mataifa mengine Duniani katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo ambapo zaidi ya watoto elfu mbili mia tano nchi nzima hugundulika kuwa na tatizo la ulemavu wa mguu kifundo kila mwaka hapa nchini.

Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma Sambamba na Ufunguzi wa Cliniki ya kutibu Dkt.Kiologwe amesema kuwa jamii inatakiwa kubadilika na kuacha tabia ya kuwaficha na kuwanyanyapaa watoto wenye Ulemavu huo.

Aidha amewapongeza wakina mama walioitikia wito na kupeleka watoto wao wenye changamoto ya mguu kifundo, pamoja na wadau waliodhamini maadhimisho hayo ikiwemo TCCO kwa kuchagua mkoa wa Dodoma kama sehemu yakwanza kuadhimisha maadhimisho ya watoto wenye ulemavu wa mguu kifundo.

Pamoja na hayo amepongeza taasisi mbalimbali kwa kushirikiana na TCCO, kwani wamesaidia kuwaondolea adha watoto pamoja na vijana ambao walikuwa wanaishi kwenye mazingira ya unyanyapaa lakini wafadhili kwa kushirikiana na TCCO pamoja na wadau mbalimbali wamerejesha heshima ya utu wa mwanadamu.

Ameongeza kuwa TCCO imeshahudumia watu zaidi ya elf nne, ambao wamefanyiwa marekebisho ambapo ni watanzania wengi wamerejeshewa heshima yao ya utu pamoja na mwonekano.

“ Pongezi nyingi ni kwaajili ya nia iliyomo mioyoni mwetu lakini nilikuwa nawaambia watu kazi ya utabibu ni zaidi ya kazi ya uaskofu na nizaidi ya kazi ya upadre sisi tunamwangalia mtu kwa ujumla wake” amesema Dkt. Kiologwe

Pia Dkt. Kiologwe ameeleza kuwa thamana waliopewa matatibu ni kubwa kwani kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwa mwanadamu Daktari pekee ndiyo mwenye kutekeleza shughuli zote hizo hata pale inapohitajika kumrekebisha madaktari hufanya hivyo pia wanawashukuru wote waliojitokeza kushiriki maadhimisho hayo.

Aidha amesema kuwa TCCO wanajumla ya matawi 35 kote nchini (kliniki), ambapo Dkt. Kiologwe ameomba taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali kuanzisha kliniki kwenye kila mkoa na wilaya kwani takribani katika kila watoto elf moja wanaozaliwa mtoto mmoja anazaliwa na mguu kifundo.

Awali akizungumza amesema kuwa changamoto ya ufanisi imekuwa tatizo kubwa sana kwa watoto wenye ulemavu wa mguu kifundo hasa kwenye utendaji wa kazi, elimu, kushiriki kwenye masuala ya uchumi pia adha ya kuishi kwenye jamii.

Ambapo ni wastani wa watoto 120, kwa mwaka wanazaliwa kwenye mkoa wa Dodoma peke yake wakiwa na ulemavu wa mguu kifundo ikiwa ni pamoja na kukumbana na adha ya kwenda kwenye matibabu ambapo watu wengi wamezoea masuala yote yanayohitaji marekebisho yanafanyika kwenye hospitali ya CCBRT, ambayo pia ni msaada mkubwa katika nchi kwani elimu kuhusu wapi matibabu ya ulemavu wa mguu kifundo yanapatikana hivyo elimu yakutosha inatakiwa kutolewa kwa umma ili kujua ni wapi matibabu ya ulemavu wa mguu kifundo yanapatikana.

Pia ameeleza changamoto ambazo zinapelekea watu kushindwa kupata matibabu hayo ni pamoja na kipato, ambapo kwa uzinduzi wa kliniki hiyo ya marekebisho ya mguu kifundo yatakuwa yanafanyika kila alhamisi na kwa watoto wote chini ya umri wa miaka mitano matibabu yatakuwa bure.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano wa Wadau wanaojihusisha na Matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina amesema kuwa bado kuna changamoto miongoni mwa jamii wakihusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina ambapo amesema wanaendelea kutoa Elimu kwa jamii ili iache kuwanyanyapaa watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo.

''Rai yangu kwa wazazi/walezi pamoja na wananchi kiujumla waache kuwafungia na kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani tatizo hilo linaponyeka hivyo jamii iache tabia ya kuwanyanyapaa pamoja na kuhusisha ugonjwa huu kwa imani za kishirikina''amesema Dkt.Mhina

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wazazi wenye watoto wenye matatizo ya mguu Kifundo wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyapaa miongoni mwa jamii hivyo wameiomba Serikali kufanya msko na kuwachukulia hatua baadhi ya wazazi wanaowaficha watoto wenye matatizo hayo ya Ulemavu

 
Share To:

Post A Comment: