Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inategemewa kusafiri leo kuelekea
Misri ambako itaweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afcon.
.
.
Stars inasafiri na nyota 32 huku Nyota 7 wakiachwa. Nyota walioachwa ni
Jonas Mkude, Ibrahim Ajib, Ayoub Lyanga, Ally, Khamis, Kennedy Wilson na
Shomari Kapombe.
.
.
Kocha Amunike amesema kigezo kilichotumika kuwaacha nyota hao ni
perfomance yao mazoezini na nidhamu huku akisisitiza anajua watu
wanamatamanio yao juu ya wachezaji fulani lakin nidhamu na utimamu wa
viwango vyao ktk mazoezi ni kipaumbele kikubwa mbali ya Kapombe ambaye
bado hajawa fiti.
.
.
Aidha Amunike amesema amewajumuisha makinda Kelvin John na Boniphace ili
kuwapa uzoefu zaidi akitambua umuhimu wa kuimarisha vijana kwa soka la
baadae.
Post A Comment: