MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya Jijini Tanga Omari Athumani Futari kushoto ambapo vitu viliyotolewa na Mchele kilo
100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo
50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo
walikabidhiwa
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye
pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia
akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya
Jijini Tanga Omari Athumani Futari kushoto ambapo vvitu viliyotolewa na Mchele kilo
100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo
50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo
walikabidhiwa
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari mmoja wa wanafunzi wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa Imamu Abdallah
Sehemu ya Shehena ya futari ilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa ajili ya Taasisi kubwa nne za Kiislamu Jijini Tanga
Sehemu ya Shehena ya Futari iliyotolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) kwa Taasisi nne kubwa za Kiislamu Jijini Tanga
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga
(CCM) Ummy Mwalimu ametoa shehena ya futari kwa Taasisi kubwa za nne za Kiislamu Jijini
hapa kwa ajili ya matumizi kwenye mwezi mtukufu wa ramadhani
Taasisi ambazo zimepata futari hiyo
iliyotolewa na Mbunge Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ni Shamsi Maarifa Zaharau,Maawal na Tamta ambapo halfa ya
makabidhiano hayo yalifanywa na kwenye taasisi zao.
Futari iliyotolewa na Mchele kilo
100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo
50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo
walikabidhiwa
Akizungumza baada ya kukabidhi
futari hiyo Waziri Ummy alisema ameona atoe futari hiyo kwa taasisi hizo kubwa
kwa niaba ya wakazi wa mkoa wa Tanga akiwa kama kiongozi wa mkoa huo kwenye
kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Nikiwa kama mwana jamii na kiongozi
wa mkoa wa Tanga nimeona nitoe futari kwa taasisi hizo kubwa nne kwa niaba ya
wakazi wa Tanga ambazo zinafundisha vijana wetu kutoka maeneo mbalimbali elimu
ya dini na mambo yanayohimizwa kwenye dini kwani shamsi maarifa ina wanafunzi
600,zaharau wanafunzi 200“Alisema.
Aidha pia aliwataka waislamu mkoani
Tanga kuendelea kutenda mambo mema kwenye mwezi mtukufu wa ramadahani na
kuendelea kuyatenda hata baada ya kumalizika mwezi huo ikiwemo kufanya ibada
kila wakati.
Awali akizungumza mara baada ya
makabidhiano hayo Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa iliyopo Duga
Jijini humo Omari Athumani alimshukuru Waziri Ummy huku wakieleza wamepata mtu
wa pekee Tanga kutokana na kuwa karibu na wananchi kila wakati kwa kutoa
misaada.
Alisema kwamba hii sio mara ya
kwanza kutokana na kwamba amekuwa akiwajali wananchi kwa kujitolea vitu
mbalimbali wakati wa mwezi mtukufu wa ramadani na hivyo ni wazi kwamba tumepata
mtu wetu sahihi kwa mkoa wa Tanga.
“Tuna mshukuru Mwenyezi Mungu
akuongoze kwenye kazi zako na aendelee kukupa afya njema wewe a kubwa
wataendelea kuliombea Taifa Amani na kumuombea Afya njema Rais wetu Dkt John
Magufuli na kumtakia mafanikio katika kuliongoza Taifa”Alisema
Mwisho.
Post A Comment: