Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Viongozi wa
dini kutoka makanisa mbalimbali mkoa wa Arusha wamehitimu mafunzo ya udereva na
usalama barabarani yaliyotolewa na Chuo cha Wide Institute of Driving lengo ikiwa ni kudhibiti ajali zinazosababisha
vifo na majeruhi.
Mkufunzi wa
Chuo hicho Faustine Matina amesema kuwa
mafunzo hayo yalifanyika kwa umakini mkumbwa kwa viongozi hao wa dini ili
waweze kuwa mabalozi wa masuala ya usalama barabarani na kuokoa maisha ya watu.
Matina
amesema kuwa viongozi hao wa dini wamehitimu mafunzoyao na kupatiwa vyeti hivyo
kukidhi matakwa ya serikali ya kuwataka madereva kuwa na vyeti vya shule ya
udereva pamoja na leseni kama vigezo muhimu kwa madereva.
Mkuu wa
Kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha Joseph Bukombe amewataka
viongozi hao wa dini kuhubiri masuala ya usalama barabarani katika makanisa yao
ili kuokoa maisha ya waumini wao ambao wengi ni madereva.
“Nawaomba
msikae kimya mkazungumze huko makanisani badala ya kusema nendeni kwa amani
muwaambie kuwa wasisahau kufunga mkanda wanapokua kwenye magari yao kwa kufanya
hivyo tutaokoa maisha yao” Alisema Bukombe
Mwakilishi
wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha
ambaye ni Mrakibu wa polisi Makao Makuu ya polisi Arusha Namsemba
Mwakatobe amesema kuwa jeshi hilo litashirikiana na viongozi wa dini katika
kutatua changamoto za usalama barabarani pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Makanisa Mkoani Arusha ,Askofu Stanley Hotay amesema kuwa mafunzo
hayo yatawasaidia Viongozi wa dini kuwa na uelewa mkubwa na kujifunza vitu
vingi ambavyo walikua hawavijui kuhusu usalama barabarani.
Post A Comment: