Waziri
wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua
Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum
Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Wa nne kulia) akifatilia mada
mbalimbali mara baada ya kufungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi,
lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019.
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua
Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum
Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019.
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japheth Hasunga (Wa nne kulia) akifatilia mada
mbalimbali mara baada ya kufungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi,
lililofanyika katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Mei 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Kumekuwa
na mwamko mkubwa na muitikio mahusiusi wa vijana kuingia katika
shughuli za kilimo tofauti za siku za nyuma ambapo ilikuwa ni vigumu
kukuta vijana wakishawishika kuingia katika kilimo.
Takwimu za mwaka 2014 za Integrated Labour Force Survey chini
zinaonesha kwamba vijana ni asilimia 56 ya nguvu kazi ya Taifa. Hivyo,
wakihusishwa na kuwezeshwa ipasavyo kwa kuwavutia kwa kuzingatia
mahitaji yao ya msingi katika kuwekeza katika kilimo, vijana hawa
watalifikisha Taifa katika maendeleo chanya.
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japheth N. Hasunga (Mb) ameyasema hayo Leo Tarehe 23 Mei
2019 wakati akifungua Jukwaa la Fikra la Mwananchi, lililofanyika
katika ukumbi wa Milleinum Tower Jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa Wizara ya Kilimo ina Mkakati wa Taifa wa Vijana wa kuwawezesha
kushiriki katika kilimo kwa kuzingatia malengo makuu kumi (10) yakiwemo
upatikani wa ardhi, upatikanaji wa mitaji, mafunzo ya ujasiriamali na
uhakika wa masoko ya bidhaa zao.
“Swali
kubwa na msingi hapa ni je, sisi wadau wote kwa ujumla tunayatekeleza
haya ili kuwavutia vijana kuweza kushiriki uwekezaji katika kilimo
kupitia mnyororo wa thamani? Kwani tunakwama wapi?” Aliuliza Mhe Hasunga
Alisema kuwa ili kufikia
malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 ya kufikia uchumi wa kati wa viwanda
kunahitajika kilimo bora kitakachowezesha upatikanaji wa malighafi za
kutosha kutumika katika viwanda.
Vilevile,
Kilimo chenye tija pia kitawezesha kipato cha wakulima kuongezeka na
hivyo kuwezesha wananchi wengi kufikia kipato cha kati. “Nina uhakika
ifikapo mwaka 2025 tunaweza kufikia uchumi wa kati na pengine na kuzidi
kiwango hicho tulichojiwekea na hapo tutaiona Tanzania mpya yenye neema”
Alisema
Mhe
Hasunga alieleza kuwa Wizara ya Kilimo imeanza kufanya marekebisho ya
Sera ya Kilimo na kutunga Sheria ya Kilimo, hatua ambazo zitaimarisha
usimamizi na kutoa mwongozo wa maendeleo ya sekta ya kilimo kwa ujumla.
Kongamano hilo pla Jukwaa la Fikra au Mwananchi Thought Leadership Forum (MTLF) lilirushwa
mubashara na Kituo cha Matangazo cha ITV pamoja na Radio One Sterio
likiwa na lengo la kujadili masuala yanayowagusa Watanzania moja kwa
moja kwa lengo la kuyatafutia suluhisho kwa pamoja kupitia mijadala
iliyotolewa.
Alisema
tangu majukwaa ya namna hiyo yalipoanza mwaka 2018 yakihusisha pia IPP
Media (ITV, Radio na Capital Radio) masuala kadhaa yamejadiliwa ikiwa
pamoja na mada za kuvutia kama vile "Magonjwa Yasiyoambukiza", mada ya
"Tanzania ya Viwanda" na masuala ya Mazingira. Kupitia jukwa hili,
Mamilioni ya Watanzania wamefaidika kwa kutoa na kusikiliza maoni katika
Nyanja hizo kupitia mitandao ya jamii, televisheni, radio na magazeti.
Mhe Hasunga alisisitiza kuwa Serikali
haiwezi kufikia malengo yake bila kuwashirikisha wadau, aliwakaribisha
wananchi na wadau wote kujadili na kutoa mawazo yatakayo iwezesha wizara
ya kilimo kutoka katika hali iliyopo na kwenda hali nyingine ya
kuboresha kilimo katika nyanja za masoko, upatikanaji wa pembejeo,
wataalamu na zana bora za kilimo.
Waziri
Hasunga aliongeza kuwa Pamoja na umuhimu wa sekta ya kilimo katika
kuchangia uchumi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko sekta zingine, kuajiri
watu wengi zaidi kuliko sekta nyingine, kuwezesha upatikanaji wa chakula
cha kutosha hapa nchini na ziada kuuza nje ya nchi, kuchangia fedha
nyingi za kigeni na kuwa moja ya sekta mama katika pato la Taifa na
nguzo kuu ya uchumi, bado kilimo hakijaweza kukuza uchumi wetu kwa namna
inavyostahili kutokana na umuhimu wake.
“Tunatambua
kihistoria kuwa nchi nyingi duniani zilianzia maendeleo kwenye
mapinduzi ya kilimo, kwenda mapinduzi ya viwanda, huduma na baadaye
teknolojia. Pengine hatuwezi kukwepa kufanya mapinduzi hayo ya kilimo
hapa nchini. Tutakachoweza kufanya ni mapinduzi ya kasi zaidi kwa sababu
tuna mifano mingi ya kuiga hapa duniani” Alikariiriwa Mhe Hasunga
MWISHO
Post A Comment: