Katibu
Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongoza kikao kazi
cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa
utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga
(Expanding Rice Production project), Kilichofanyika Jijini Dar es salaam
tarehe 22 Mei 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Katibu
Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameengoza kikao kazi
cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa
utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga
(Expanding Rice Production project), mradi ambao unatekelezwa Tanzania
bara na Zanzibar.
Kikao
hicho cha majumuisho kimefanyika leo leo Tarehe 22 Mei 2019 katika
ukumbi wa ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo 1 Jijini
Dar es salaam.
Ujumbe
huo kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Bi Sarah Simons umeeleza
kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi katika utekelezaji wa kazi za mradi
huo kulingana na malengo yaliyowekwa kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita.
Ujumbe huo ulianza kazi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mradi huo wa ERPP tarehe 19-21 Mei 2019 ambapo walitembelea Tanzania bara na Zanzibar na walikutana katika wizara ya Kilimo (Bara) na
Wizara ya kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi (Zanzibar) na wameshukuru
ushirikiano walioupata kwa watendaji wanaosimamia mradi huo.
Aidha ujumbe huo pamoja na kusisitiza kasi ya utekelezaji
na ukamilishaji wa kazi za Mradi huo pia waliridhishwa na namna ambavyo
mradi umekuwa ukiripoti kuongezeka kwa uzalishaji wa mpunga kwa hatua
za awali baada ya wakulima kutumia mbegu bora katika mfumo wa kilimo shadidi (SRI).
Pia
maendeleo mazuri katika maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya
Umwagiliaji na Maghala kwa kipindi cha miezi sita iliyopita na wamekuwa
na matumaini kuwa Ujenzi wa miradi hiyo na kazi zingine zitakamilika
kabla ya tarehe ya mwisho ya mradi huo.
Mhandisi
Mtigumwe (Katibu Mkuu Kilimo Tanzania bara) ameushukuru ujumbe huo na
kuwaeleza kuwa wataendelea kwa kasi kutekeleza shughuli zilizobaki za
mradi huo ili tija kwa wakulima na nchi ionekane.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na
Uvuvi Bi Mansura Kassim aliushukuru Ujumbe huo kwa ufuatiliaji wao na
kueleza kuwa Kwa upande wao wataendelea kukamilisha kazi zilizobakia
katika mradi na kusimamia mradi huo ipasavyo.
MWISHO.
Post A Comment: