Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Benki
ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge,
Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa
NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert Jonkergouw katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JUMAMOSI, MEI 25, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Albert Jonkergouw katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi, wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Benki
ya NMB kwa Masheikh wa Mikoa ya
Kanda ya Kati, Wazee wa Dodoma, Wabunge, Viongozi wa Dini, Wananchi,
wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na wafanyakazi wa NMB kwenye hoteli ya
Dodoma, Mei 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watumie Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani kwa kudumisha amani na mshikamano na kuwaombea viongozi wa
kitaifa.
“Mwezi
huu tuna majukumu makubwa ya kufanya ibada, kutubu dhambi zetu na
kuomba rehma kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kudumisha mshikamano na kuwa
wavumilivu.”
Waziri
Mkuu alitoa wito huo jana jioni (Ijumaa, Mei 24, 2019) aliposhiriki
hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya NMB iliyofanyika katika Hoteli
ya Dodoma.
Alisema
kila wananchi aendelee kuliombea Taifa lizidi kudumisha amani na
mshikamano. “Tuhakikishe tunatenda matendo mema yenye kumpendeza
Mwenyezi Mungu.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuipongeza benki ya NMB kwa huduma bora
wanazozitoa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwa na matawi mengi hadi
vijijini.
Awali, Mkurugenzi wa benki ya NMB, Albert Jonkergouwalisema lengo la kuandaa hafla hiyo ya futari ni kuimarisha ushirikiano uliopo baina yao na wateja wao.
Mkurugenzi
huyo alisema katika kipindi hiki Waislamu wanapaswa kumrudia Muumba wao
na kumshukuru kwa mema yote anayowajalia waja wake.
“Mwezi
wa Ramadhan ni kipindi muafaka cha kufuturu pamoja hivyo, nawashukuru
wateja wetu kwa kujumuika nasi nawaomba muendelee kutumia huduma zetu.”
Alisema mkusanyiko huo unadhihirisha kuwa wao ni sehemu ya jamii ya Watanzania wote, hivyo aliwasisitiza wateja wa benki hiyo waendelee kutumia zaidi huduma za kidijitali.
Hafla
hiyo ilihudhuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia
Ackson, Mashekhe wa Mikoa ya Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na
Manyara).
Wengine
ni Wazee wa Dodoma, Waheshimiwa Wabunge , Viongozi wa dini, wananchi,
Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali na Wafanyakazi wa NMB.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma,
Post A Comment: